Ni bahati au mafanikio ya TFF ya Karia

hana lolote faida iliyopo sasa hivi kwa stars ni kwamba CAF inapanga mashindano kwa kanda ndiyo maana tunafanikiwa kwa kukutana na timu mbovu za ukanda wetu
 
Ni uongozi wa sasa TFF chini ya Mwenyekiti Karia,Mwenyekiti si mtendaji sana lazima pale TFF kuna masterminds pembeni.Nchi kuonekana kwenye mashindano ya Kimataifa mara kwa mara ni mafanikio.CHAN si michuano midogo pia
Karia ni kiongozi mzuri anayejua anachokifanya .Kumbuka alianza kuchomoza kipindi Cha Tenga akiwa mwenyekiti bodi ya ligi pia ni mtumishi wa umma. Pia alifanya kazini na Malinzi Kama makamu wa Rais. Makamu wake Athumani Nyamlani pia alifanya kazi na Tenga Kama makamu wa Rais,ni mzoefu katika uongozi wa mpira lakini pia anajua fitina za mpira( Master mind mzuri tu).Pia viongozi wengine amewachagua kwa usahihi. Kwa hiyo alama/mfumo wa style za uongozi wa Tenga bado unaishi.
Ni watu wanaofanya kazi zaidi kuliko kutafuta sifa za magazetini.

Na mwisho kukamatwa na kutulizwa kwa watu wenye fujo Kama kina Malinzi,Wambura,Aveva,Hanspope,Manji n.k kumesaidia kurejesha utulivu kwenye sekta ya mpira wa miguu. Kwa hiyo Serikali pia imechangia
 
Tukisema ni jitihada za karia na genge lake itakuwa ni vichekesho kama vile walikuwa wanatutumia tigo/voda zamani

ni upepo tu wala hakuna mikakati ya kufaulu yote hayo,mataifa africa tumepita kwa kubebwa na ug. hii ya cameroon pia bahati

kuhusu hao madogo, kitambo tu walisha anza kufanya poa sema kdg bashite kahamasisha kiasi ila karia bwege tu hana mkakati wala mchango kwenye hayo mafanikio
 
Anakula matunda ya watangulizi wake.
 
Watu sijui hamjui au mnajitoa ufahamu, Tz ku-host mashindano ya under 17 ilifanikishwa chini ya ya Malinzi, hii timu ya under 17 ni mkakati uliojengwa toka malinzi, ushirika wa AFCON was purely political, siyo kitu ya kusifia. Suala la kuruhusu uwekezaji na hatimaye MO kuwa Simba ndiyo kilichoifanya Simba iimarike na nibmazingira yaliyowekwa toka enzi za Malinzi.
 


Tatizo la Wa-TZ wengi ni kutotaka kuona na kutambua mafanikio ya wengine,hata inapotokeo kuna matokeo chanya,hutafuta njia kukwepesha uhalisia. Ndolanga,Tenga,Malinzi na wengine walikuwepo. Jitihada zao zilionekana kwa kadri ya uwezo wao.
Na Sasa ni Karia na wenzake wapi nao jitihada zao zinaonekana.Tunapaswa kutambua jitihada zao
 
Tunaomba utuanishie hizo jitihada ni zipi zilizofanywa na TFF ya Karia, ukiachana na swala la uteuzi wa makocha?
 
Tunaomba utuanishie hizo jitihada ni zipi zilizofanywa na TFF ya Karia, ukiachana na swala la uteuzi wa makocha?
Mkuu, sie mashabiki wa soka tunachojali ni ushindi, hiyo ndio furaha yetu.Siwezi kuainisha jitihada za TFF kwa kuwa sipo kwenye taasisi hiyo.
 
Tunaomba utuanishie hizo jitihada ni zipi zilizofanywa na TFF ya Karia, ukiachana na swala la uteuzi wa makocha?
Anasimamia kwa weledi pesa za fifa kiasi ataanza kujenga kituo cha michezo mnyanjan Tanga
 
karia hana lolote zaidi ya kulundika wanaSimba TFF!!
 
Mkuu, sie mashabiki wa soka tunachojali ni ushindi, hiyo ndio furaha yetu.Siwezi kuainisha jitihada za TFF kwa kuwa sipo kwenye taasisi hiyo.
Sasa utasemaje kuwa kuna jitihada za TFF ya Karia zilizopelekea kupatikana kwa matokeo chanya wakati haujui hizo jitahada ni zipi walizozifanya?
 
Anasimamia kwa weledi pesa za fifa kiasi ataanza kujenga kituo cha michezo mnyanjan Tanga
Kwahiyo mafanikio ya timu ya Taifa na timu ya Simba tunayojadili hapa yametokana na hii jitihada ya TFF kutaka kujenga kituo cha michezo Tanga?
 
Subiri watu wa Yanga waje kuponda, sijui kwanini watu wa Yanga wanamtazama Karia kisimbasimba, basi wanaponda kila kitu cha uongozi wa Karia.
Wabongo tunafeli hapa tu, kimeulizwa kitu kingine kabisa majibu yametoka ya kukurupuka
 
Ni mafanikio ya Utawala wa Karia.
Kwa Mara ya pili tumeweza kucheza mashindano ya African Championship tukiwa kundi moja na jirani zetu Kenya.
Hongera Karia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…