M-bongotz
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 1,736
- 408
Wakuu nipo kwenye mchakato wa kuchukua mkopo toka Benki yeyote, mkopo ninaohitaji ni personal loan ambayo watakuwa wananikata kwenye mshahara wangu, nimejaribu kufuatilia mabenki kadhaa lakini riba zao zinaumiza sana kwa mfano Barclays Bank wao wanatoza riba ya 23% ambayo kwa maoni yangu ni kubwa sana. Kama kuna yeyote mwenye uzoefu na masuala haya ya mikopo na riba tafadhali anijulishe (pia ni kwa faida ya wengine) ni benki gani hapa nchini inayotoa riba nafuu kwa mikopo binafsi.
Nawasilisha.
Nawasilisha.