Ni benki gani Tanzania ipo haraka katika kufungua akaunti?

UTASHI

Senior Member
Joined
Jan 19, 2013
Posts
135
Reaction score
56
Habari wote na poleni na majukumu ya kila siku,.
Naomba kuuliza,Hivi ni benki gani Tanzania mtu unaweza kufungua akaunti na ukapata ATM kadi yako siku hiyo hiyo na kuweza kuitumia,yaani bila kuelezwa habari ya kusubili na kuja kuchukua kadi yako siku nyingine?
Asante!
 
nenda crdb, wana kitu yao inaitwa fast account opening (FAO) unapata kila kitu hapo hapo. hata NMB pia (chap chap account), ila hawana visa wala mastercard, kadi zao zinatumika kwenye ATM zao tu. ila za crdb unatumia atm yoyote yenye visa au mastercard popote pale.
 
Waone First National Bank (FNB),fasta ATM hapo hapo na kila Transaction utakayofanya unapata sms notification.
 
Nenda Equity Bank ndani ya dakika 10 usafungua akaunti pia branch zao hasa pale QUALITY CENTRE wanaoperate mpaka usiku.
 
Crdb ni kiboko,nilifungua akaunti papo hapo mpaka nikafikiri labda mtoa huduma ananitania,hongera sana crdb,kweli ulipo tupo na unakuwepo kwa wakati
 
Benki ambayo utachukua wiki mpaka miezi ni twiga bancorp,hapa sikushauri,ni ka benki ka hovyo,very archaic,hakana hata sim banking yaani hovyo kabisa
 
nenda crdb, wana kitu yao inaitwa fast account opening (fao) unapata kila kitu hapo popote pale.

waone first national bank (fnb),fasta atm hapo hapo na kila transaction utakayofanya unapata sms notification.

nenda equity bank ndani ya dakika 10 usafungua akaunti pia branch zao hasa pale quality centre wanaoperate mpaka usiku.

pbz
people bank of zanzibar

du mabenki yana watu hadi jf...kweli kiboko...
 
Benki ambayo utachukua wiki mpaka miezi ni twiga bancorp,hapa sikushauri,ni ka benki ka hovyo,very archaic,hakana hata sim banking yaani hovyo kabisa
hahahah kweli alafu hapo wana huduma ya money gram kila nkienda netwrk down siku mbili mfulululizo mpaka aliyekua anatumiaga hela nkamwambia basi mzee imetosha, twiga bankcorp kimeo kweli hata kwa huduma zao
 
kiukweli bado sijaona benki ambayo ipo makini kama benki za wakeya (KCB na EQUITY) lakini njuavyo watanzania wakisikia chochote kuhusu kenya povu linawatoka sana
 
kiukweli bado sijaona benki ambayo ipo makini kama benki za wakeya (KCB na EQUITY) lakini njuavyo watanzania wakisikia chochote kuhusu kenya povu linawatoka sana

KCB wapo vizuri sana.Hasa Tawi La Zanzibar.
Lakini tawi la Samora pale kuna wazembe wanajiona kama wapo wapi sijui wakati pesa zetu ndio zinawaweka pale.
Pale tu ndio niliona doa,wapo slow kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…