Ni biashara gani naweza kuifanya kwa Mtaji wa million 25

Ni biashara gani naweza kuifanya kwa Mtaji wa million 25

Elezea zaidi hiyo maliasili mkuu
Tunapigaje pesa
Tuonyeshe njia
Kwenda porini kubeba magogo yaliyotolewa mabanzi.

Kinachobaki kinaitwa slipa sasa hizo ndio unapeleka sokoni.

Kumbuka vibali ni muhimu kwa usalama wa pesa yako.Usipende short cut kwenye hiyo biashara.
 
Tafuta eneo ambalo viwanja ndio vinajengwa/ jengeka .... nunua hata 20x20 weka machine ya kupiga tofari

Unanunua cement tone 30 weka pale

Uza nondo ring box, kodisha mbao rundo la Kokomo uza kidg kidg weka na misumali etc

Hela inabakia unaongeza mambo kidg kidg huku hardware yako inakua
 
Hapo usitake uweke 25 yote tafta biashar ambayo ipo rohon weka ata 3 m tyuu badae utakua unaongeza mdg mdg unatanua biashara sasa
 
Hapo usitake uweke 25 yote tafta biashar ambayo ipo rohon weka ata 3 m tyuu badae utakua unaongeza mdg mdg unatanua biashara sasa
Kama biashara gani mtu anaweza Anza na mtaji wa million 3 na huku biashara ikakua
 
Wakuu ushauri wenu ni muhimu. Ni biashara gani naweza kuifanya nikiwa na kiasi cha tsh million 25? Naamini kwa ushauri wenu na wengine watajifunza kitu hapa.

Ahsante.
Hiyo 25M umeipataje ?
Halafu ukose biashara ya kufanya??
 
Hiyo 25M umeipataje ?
Halafu ukose biashara ya kufanya??
Mkuu kuna sababu nyingi sana za kupata pesa nyingi bila ya kuhangaika Sana. Mfano urithi, betting, kuokota pesa. zote hizo zinaweza kukufanya ukawa millionaire kwenye wallet ila maskini kichwani.
Hivyo ukiwa na wazo la kumkomboa kijana mwenzako kiuchumi usiache kumshirikisha Kwa sababu kama ulizouliza
 
Kama biashara gani mtu anaweza Anza na mtaji wa million 3 na huku biashara ikakua
Best Kwang ni biashar yoyte ya jumla yaaan biashar ya kununua na kuuza kitu kwa bei ya jumla mfano kutoa dagaa mwanza kupeleka nje kama dar dom songea mbeya n.k au hata samaki unaanza kwa kwa hela kidg ata mil 2 tyu ukiona inalipa unaongeza tena mbili ila ni vzur magazine yako yalipo ndoo ikawa pia sehem ya kufikia mzigo wako
 
Mkuu Nipo mkoa wa rukwa wilaya ya sumbawanga.
Kwa mtaji wa TZS 25 milioni, kuna fursa nyingi za biashara ambazo unaweza kufikiria kuanzisha Tanzania. Hapa kuna baadhi ya mawazo ya biashara ambayo yanaweza kufaa

1. Biashara ya Vyakula (Mgahawa/Mama Ntilie)
- Unaweza kufungua mgahawa au biashara ya chakula cha haraka. Chakula ni hitaji la msingi, na wateja watakuwa wa uhakika hasa kama utachagua eneo lenye watu wengi kama vile mjini, maeneo ya ofisi, au karibu na shule na vyuo.

2. Kilimo cha Mboga na Matunda
- Kilimo cha mboga na matunda ni biashara yenye faida nchini Tanzania. Unaweza kuwekeza kwenye kilimo cha matunda kama vile machungwa, maparachichi, au mboga kama vile nyanya na pilipili hoho.

3. Biashara ya Maduka ya Rejareja
- Kufungua duka la bidhaa za rejareja kama vile vifaa vya nyumbani, bidhaa za chakula, au mavazi. Chagua eneo lenye wakazi wengi ambapo unaweza kupata wateja wa kutosha.

4. Biashara ya Urembo na Vipodozi
- Unaweza kuanzisha duka la vipodozi, bidhaa za urembo, au saluni ya urembo kwa wanawake na wanaume. Urembo ni soko linalokua haraka nchini Tanzania.

5. Biashara ya Usafiri
- Kama vile bodaboda au bajaji. Hii ni sekta inayokuwa kwa kasi kutokana na hitaji la usafiri wa haraka na rahisi katika miji mikubwa.

6. Biashara ya Ufugaji
- Ufugaji wa kuku wa nyama au mayai unaweza kuwa na faida nzuri, hasa ukizingatia kuwa nyama ya kuku ni maarufu sana nchini Tanzania.

7. Biashara ya Teknolojia na Huduma za IT
- Unaweza kufikiria kufungua kituo cha huduma za IT, kama vile matengenezo ya simu na kompyuta, kufunga na kuuza vifaa vya teknolojia, au kutoa huduma za mafunzo ya IT.

8. Biashara ya Utalii wa Ndani
- Ukiwa katika eneo lenye vivutio vya utalii, unaweza kuanzisha biashara ya kutoa huduma za utalii kama vile ziara za maeneo, hoteli ndogo, au shughuli za kitamaduni kwa watalii.

9. Biashara ya Ufundi (Workshop)
- Kufungua karakana ya magari, baiskeli, au vifaa vingine vya ufundi. Utaweza kuwahudumia wateja wengi hasa ikiwa utatoa huduma nzuri na za uhakika.

Kabla ya kuanza, ni muhimu kufanya utafiti wa soko ili kuelewa mahitaji halisi ya wateja katika eneo unalotaka kuanzisha biashara yako. Pia, hakikisha una mpango mzuri wa biashara na ufuatiliaji wa matumizi ili kuhakikisha mtaji unatumika kwa ufanisi.
 
Wakuu ushauri wenu ni muhimu. Ni biashara gani naweza kuifanya nikiwa na kiasi cha tsh million 25? Naamini kwa ushauri wenu na wengine watajifunza kitu hapa.

Ahsante.
Kama haujui bors kaweke utt utakula hasara tu
 
Wakuu ushauri wenu ni muhimu. Ni biashara gani naweza kuifanya nikiwa na kiasi cha tsh million 25? Naamini kwa ushauri wenu na wengine watajifunza kitu hapa.

Ahsante.
Biashara zipo nyingi sana za kufanya ila ni vyema ungesema biashara ambayo ushawai kuifanya au ungependekeza mwenyewe hata biashara tano tofauti ili wana jamvi tukupe mbinu kutokana na uzoefu wetu kwenye izo biashara.


Kama haujawahi kufanya biashara yoyote basi nakushauri ufanye biashara yoyote ile ya chakula au kitu kinacholika.

Mfano.
1)Mahindi
2)Maharage
3)Mchele
4)Viazi mviringo
5)Dagaa

Hizo biashara zote ni kwa mtu mwenye mtaji mkubwa kama wako, ila hizo biashara ni za jumla na inatakiwa kujitoa kukusanya taarifa sahihi ili ukizifanya usipate hasara.

Ila kumbuka biashara inahitaji uvumilivu ili uwe na uzoefu wa kufanya vizuri.

Pia kuna biashara nyingine kama:-

Mikopo (vikoba)
Vipuri (pkpk au gari)
Duka la dawa


Hayo ni machache kati ya mengi ambayo unaweza kufanya na ukanufaika.
 
Tupe mrejesho uliamua kufanya biashara ipi watu wajifunze
 
Back
Top Bottom