Ni biashara gani ndugu zangu inaweza kuniingizia elfu saba kwa siku?

Ni biashara gani ndugu zangu inaweza kuniingizia elfu saba kwa siku?

Sauda

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2018
Posts
860
Reaction score
1,106
Nimepiga mahesabu yangu ya maisha, kwa kuanza nahitaji walau elfu 9 Mpaka 10 kwa kila siku niiweke.

Biashara gani itanipatia wastani wa Elfu 9-10 kwa kila siku?
Nataka nijiajiri.

Hapa nina mtaji wa laki mbili cash. Naweza kuongeza hata ikafika laki tatu, ila niwe na uhakika wa kupata elfu kumi kwa kila siku kama faida.

Naweza kwenda kuishi Mkoa wowote Tanzania, ila hela hiyo uhakika wa kuipata uwepo.
Nisaidieni...

Mtaji; Laki mbili
Hela ninayotaka kuingiza; Wastani wa elfu kumi kwa siku.
 
Biashara nyingi ndogo ndogo kwa Dar unapata tena zaidi ya hiyo kwa siku:

1. Kandoro, Barafu, Ice cream.

2. Kukaanga mihogo.

3. Meza ya vitu vidogodogo ( Socks, Boxer, sandals etc
 
Kuandika ni rahisi sana kuliko uhalisia...
Mkuu hunijui.

Nimeuza sana mabanda unayoona yamezagaa pembezoni barabarani na njiani Kariakoo.

Nilikuwa nauza kwa kawaida tu mpaka Tsh 50K-70K kwa siku.

Ukitoa elfu 30 ukanunua vitu vilivyopungua kwenye banda lako unabaki na kama Elfu 30 mfukoni.

- Tena nilikuwa nauza vitu vya kawaida tu kama soksi, boxer, viatu vya ndani.
 
Back
Top Bottom