Ni biashara gani unaweza kufanya isiyohitaji uangalizi wa mara kwa mara?

Ni biashara gani unaweza kufanya isiyohitaji uangalizi wa mara kwa mara?

prettya

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2019
Posts
227
Reaction score
191
Salaam kwenu wote

Kama kichwa kinavojieleza, ni biashara gani mtu alie buzy anaweza fanya? Karibuni kwa mawazo tushee experience zinaweza saidia na wengine pia
 
ni biashara gani mtu alie buzy anaweza fanya?
Uuzaji/kubadilisha mitungi ya gesi (ya matumizi majumbani) na vifaa vyake, Pia waweza kuweka plates za kupikia.
1637196563064.png

Hii biashara usimamizi na hesabu zake sio pasua kichwa, hivyo itakufaa sana hii biashara, na hata kama utaweka mtu wa kusimamia wakati wewe ukiendelea na shughuli zingine zinazokufanya kuwa 'busy'.
 
Uuzaji/kubadilisha mitungi ya gesi (ya matumizi majumbani) na vifaa vyake, Pia waweza kuweka plates za kupikia.
View attachment 2014764

Hii biashara usimamizi na hesabu zake sio pasua kichwa, hivyo itakufaa sana hii biashara, na hata kama utaweka mtu wa kusimamia wakati wewe ukiendelea na shughuli zingine zinazokufanya kuwa 'busy'.
Biashara ni zaidi ya usimamizi wa hesabu. Unaweza kukuta hesabu ziko sawa lakini kauli za mhudumu zinafanya biashara inakufa. Biashara bila usimamizi ni changamoto sana.
 
Ni kweli biashara bila usimamizi wa karibu zina changamoto sana

ila sasa

Turudi kwenye mada.

Je ni biashara gani unaweza kufanya iwapo upo busy na shughuli zingine?

Ndio wazo au mawazo anayohitaji mleta mada.
Swali lake ni gumu sana, almost impossible. Kama mtu atapata hiyo biashara ambayo unaweka hela halafu na bila usimamizi unatoboa, itakuwa muujiza.

Labda ya kukopesha serikali aka government bond.
 
Salaam kwenu wote..
Kama kichwa kinavojieleza,ni biashara gani mtu alie buzy anaweza fanya?
Karibuni kwa mawazo tushee experience zinaweza saidia na wengine pia
That's good
 
Uuzaji/kubadilisha mitungi ya gesi (ya matumizi majumbani) na vifaa vyake, Pia waweza kuweka plates za kupikia.
View attachment 2014764

Hii biashara usimamizi na hesabu zake sio pasua kichwa, hivyo itakufaa sana hii biashara, na hata kama utaweka mtu wa kusimamia wakati wewe ukiendelea na shughuli zingine zinazokufanya kuwa 'busy'.
Mtaji wake inakuwa ngapi
 
Hamna Biashara ya aina hio.

Kama uko bize sana kana kwamba hautoweza kupata muda wa kufanya follow up ya mradi utakaouanzisha, bora ufungue fixed account ikiwa uko na pesa ndefu.

Biashara bila usimamizi n uongo
 
Wewe kama unataka kutokuwa na usimamizi wa karibu sana kuwa mwekezaji na sio mfanyabiashara.

Tofauti ya hivi viwili;

Mfanyabiashara anatengeneza faida kwa ku-balance gharama za ununuzi na uuzaji. Ili biashara ifanye vizuri unahitaji usimamizi wa karibu sana. mf. biashara ya huduma - hospitali, usafiri, utalii, vipuri vya magari n.k zote hizi zina changamoto tofauti tofauti ambazo ili zifanye vizuri ni lazima ziwe na uangalizi wa karibu sana.

Mwekezaji yeye anajikita kutengeneza kipato zaidi kwa ajili ya muda mrefu na sio faida. mf. unanunua eneo kama Kigamboni halafu unajenga nyumba 10 za vyumba vitatu vitatu kila moja unaweka kodi Tshs. 300k/mwezi. Hapa huhitaji usimamizi wa karibu sana. Hapa majukumu ya uangalizi, masoko na kutafuta wateja unaweza kuwapa kampuni yoyote ifanye kwa niaba yako wewe unawalipa tu commision wakati ukiendelea kufanya shunguli zingine.
 
Biashara ya kukodisha mziki,viti,mikokoteni,turubai
Hii biashara ya mziki ni nzuri ila uangalizi muhimu sa'bu wanao kodisha sana ni wa uswahilini zaidi, lkn viti na matubai hii nikweli sio lzm usmamizi , hio ya mziki kuna jamaa yangu anayo mitatu anapiga sana pesa sabu inakua na Order nyingi
 
Back
Top Bottom