Kwa nchi za wenzetu inawezekana kufungua biashara alaf unamuachia mtu ana manage wewe unasafiri kwenda kula Bata....ila siyo bongo ambapo kila mtu anayetafuta ajira anatafuta kuiba. Ukimuachia tu mtu umeisha.
Ishu sio Mahali
Haiwezekani Bongo wala huko kwa wenzetu
Ishu ni kwamba unapoamua kufanya biashara ukamweka mtu akusaidie ujue kwamba huyo mtu ana malengo yake anataka kutimiza, hakuna anayetaka kutimiza malengo ya mwenzake na yake yasitimie.
Kama ni wa kiume au wa kike anahitaji kujenga, kuoa/kuolewa, kusomesha, kusaidia nduguze nk
Kwahiyo usipomsimamia kwa ukaribu atatumia mtaji na rasilimali zako kutimiza malengo yake sio yako.
Hata ungekuwa wewe mtu amekuweka dukani unauza milioni 3 kwa siku
Huna nyumba, huna familia, ndugu zako wanakulilia shida, hujui utaenda wapi boss akisema sasa inatosha... ungefanya the same.
Pia binadamu tuna hulka ya ubinafsi, unataka uchukue kwa mwingine uweke kwako that's nature, ndio maana tunasema
Biashara yoyote ili ikue, ni LAZIMA iwe na USIMAMIZI WA KARIBU.