Ni biashara gani ya kuingiza 1000 kwa siku naweza kufanya?

Ni biashara gani ya kuingiza 1000 kwa siku naweza kufanya?

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
5,718
Reaction score
7,784
Wanajamvi nawapa salamu,

Nina mtaji wa 100,000 naomba wajuzi wanijulishe biashara inayoweza kunipa 1000 au hata 500 kwa siku. Nipo DSM

Ahsanteni nyote.
 
1.Kalanguae Mbongamboga toka kwa producers uje uuze sokoni.
2.Kodisha mkokoteni chukua miwa uuze.
3.tafuta kijiwe tengeneza chapati na mandazi uza jioni na asubuhi +uji
4.tafuta sehemu pika wali na maharage na nyama tu
5.tengeneza kachori,Bahia n mandazi uza mashuleni.
6.tafuta mahala tengeneza kibanda cha mboga mboga,nyanya,vitunguu na matunda uza.
7.tafuta bar ndogo muombe uchome mishikaki hapo mtalipana kidogo kidogo
 
Wapi wanauza kwa jumla?
Ingia kariakoo pale karibu na sheli ya Big bon upande wa ndani kidogo au ulizia kuna maduka ya wahindi wanauza hivyo vitu..

Japo niliacha wakiuza zamani kidogo so sijui bado wangalipo au hawapo.
 
kutengeneza bahasha au vile vifungashio na kuviuza madukani. huitaji mtaji mkubwa bali kujifunza tu
@diuretic bahasha zilikuwa zinafaida kabla ya hiii mifuko soft inayokaa miambili kwa pic's kuingia sokoni
 
Choma mahindi mabichi utakuja kunishukuru mzee, na utapata faida zaidi ya buku. Nenda sehemu yenye watu wengi, mfano maeneo ya sokoni, stand na mjini
 
mkuu bahasha zilikua zinaingiza mpaka 20k au zaidi kwa siku. ila soma uzi mkuu anataka buku tu au jero
Hivi ile mifuko soft naweza nikapata kwa jumla kwenye maduka gani ya VIFUNGASHIO yanapatkana mitaa ipi kwa kariakoo
 
Wanajamvi nawapa salamu,

Nina mtaji wa 100,000 naomba wajuzi wanijulishe biashara inayoweza kunipa 1000 au hata 500 kwa siku. Nipo DSM

Ahsanteni nyote.
Yaani uingize sh 500 kwa siku ukiwa DSM manake Sh 15,000 kwa mwezi! Rudi kijijini kalime
 
Yaani uingize sh 500 kwa siku ukiwa DSM manake Sh 15,000 kwa mwezi! Rudi kijijini kalime
Pole bado una mentality za kizamani. kwa taarifa yako nyakati zimebadilika na wanaolima sasa hivi ni wenye hela kwani gharama za kilimo zipo juu sana kuanzia gharama za Ardhi , pembejeo , vibarua , viuatilifu, mbolea n.k


Kama hauna pesa usitie mguu wako shamba.
 
Km uko dsm ingia K.koo Nunua mikanda ya kiume ile ambayo wamachinga wanaiuza 3000

Ukinunua kwa bei ya jumla nafkir 1000 kwa pc ...chukua hata ya 30000 hv ujaribu


Au km vp nunua drinks (soda take away, juice, maji, energy n.k) kwa bei ya jumla uwe unazunguka kule kule k.koo hukosi hela mkuu

Au Nunua mifuko kwa bei ya jumla mifuko ya size tofaut tofaut then zungusha huko huko k.koo

Au tafuta kimeza hata cha 15000 utafute sehemu yakukiweka huko huko k.koo then nunua glass protector za simu mbali mbali na covers za simu ..sema sasa kwenye hii inahitaji kidogo pia ujue na simu zipi covers na protector zinatembea haraka ( mostly ni Tecno, Infinix na aitel)

Ukiondoa aibu hiyo 100000 mbona nyingi mkuu

Note: Nasisitiza K.koo coz ndo kuna mzunguko mkubwa
 
Back
Top Bottom