Ni biashara, Mnatuhadaa mashabiki au Kuna mpinzani aliekuja kasi anawekwa mtu kati..?

mayowela

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2014
Posts
2,125
Reaction score
1,753
Kwa kumbukumbu zangu Efm huwa wanamatamasha mawili KOMAA CONCERT, na MZIKI MNENE, wamefanya kadri ya uwezo wao na mapokeo ni mazuri hasa ukipelekea matamasha yao ni bure kabisa, hawa jamaa wanafanya kweli na matamasha yao husindikizwa na shuguri nyingi kama Joging,kugawa mafuta, vipindi kurushwa nje, na Mechi ya mpira. Ni watu wasio na mbwe mbwe nyingi wala maneno ya majigambo kwa sana,

Upande mwingine kuna Tamasha la FIESTA linaandaliwa na Clouds limefanyika vizuri ila baada ya kufikia ukingoni hapo kesho kelele zimekuwa nyingi sana hasa zikitoka upande wa pili, wanasema ukubwa jalala sijaona kauli za kebehi kutoka upande huu wa Fiesta zikienda kule ila wanaonekana kuandamwa sana

Kuna Tamasha la WASAFI (Wasafi Festival), limezinduliwa dakika za mwisho wakati fiesta ikikalibia ukingoni, tamasha hili limekuja na maneno mengi ya kuwazihaki Clouds, hasa viongozi wa upande huu ndio wamekuwa kinara wakurusha vijembe ikifuatiwa na wafuasi wa upande huu kama kina Ommy Crazy na baadhi yao

Tutamatishe kwa kuangalia hizi pande tatu, Efm na Matamasha yake ni mtu anaepambana kivyake na anatengeneza base yake hanashida. Kwa Clouds na Wasafi mpaka sasa inaaminika mko kwenye marumbano makubwa, ila clouds hawajonesha majigambo yoyote wala kujibu chochote na wamebaki kudhihirisha ukomavu wao katika nyanja hiyo.
Najiuliza hivi...

Fiesta na Wasafi festival ni kitu kimoja kinachomilikiwa na mtu mmoja..?
Majigambo na Vijembe vinamalengo ya kuhadaa mashabiki na kutengeneza pesa..?
Kama si kitu kimoja Dudu Baya alitumika ili kutoa milage..?
Kama ni kitu kimoja lengo nikumdhoofisha mpinzani Efm..?
Je ni kitu kimoja ndio maana Wasafi wakapewa Ray ili afanye jingle za Wasafi festival..?

Kama sio kitu kimoja basi Wasafi mmeanza vibaya na Anguko lenu halitakuwa mbali, Kupendwa na kuwa na mashabiki wengi wanaowapenda wasanii wenu hakuwezi kwenda sawa na kupendwa kwa Kituo cha TV, Redio na Tamasha.

Ahsante.
 
Nawasubiria wajuvi wa mambo waje watufungue macho.
 
Tunasubiri hayo matamasha yaishe then tuone what next
 
Maisha ni magumu sana..matamasha ni mengi, mashabiki ni wale wale na wasanii ni wale wale...inabidi tuwakamue hao hao maan sasa kuna mtu kulala njaa hapa
 
hapa ndio nimeamini kweli ni kampuni za mtu mmoja wote wanatakiwa kupeleka mahesabu kwa bosi mara ya kwanza nilijua sauti ya bdozen kumbe ni Raymond haya mashabiki wa fiesta na wasafi endeleeni kutukanana mwisho wa siku hela zote zinarudi kwa bosi mmoja
 
kabisa
 
Ni muda wa wasanii kutojifanya wanatumika kujiingiza kwenye vita isiyowahusu!
Yasije yakawa Yale Yale ya watu kujiingiza kwenye Vinega bila kujua
 
Umesahau Ali Kiba naye ana tamasha lake huko Kahama ambalo nahic linaweza kuwa endelevu kwa mikoa mingine, Wcb hawataishia Mtwara tu lazima watazunguka na mikoa mingine....hapa ninachokiona ni Clouds wakishamaliza fiesta yao watamuunga mkono Ali Kiba kumnufaisha kupitia mgongo wa WCB, maana Kiba kaona hii ndio fursa baada ya kuanza kupotezwa.

Back
Top Bottom