mayowela
JF-Expert Member
- Nov 2, 2014
- 2,125
- 1,753
Kwa kumbukumbu zangu Efm huwa wanamatamasha mawili KOMAA CONCERT, na MZIKI MNENE, wamefanya kadri ya uwezo wao na mapokeo ni mazuri hasa ukipelekea matamasha yao ni bure kabisa, hawa jamaa wanafanya kweli na matamasha yao husindikizwa na shuguri nyingi kama Joging,kugawa mafuta, vipindi kurushwa nje, na Mechi ya mpira. Ni watu wasio na mbwe mbwe nyingi wala maneno ya majigambo kwa sana,
Upande mwingine kuna Tamasha la FIESTA linaandaliwa na Clouds limefanyika vizuri ila baada ya kufikia ukingoni hapo kesho kelele zimekuwa nyingi sana hasa zikitoka upande wa pili, wanasema ukubwa jalala sijaona kauli za kebehi kutoka upande huu wa Fiesta zikienda kule ila wanaonekana kuandamwa sana
Kuna Tamasha la WASAFI (Wasafi Festival), limezinduliwa dakika za mwisho wakati fiesta ikikalibia ukingoni, tamasha hili limekuja na maneno mengi ya kuwazihaki Clouds, hasa viongozi wa upande huu ndio wamekuwa kinara wakurusha vijembe ikifuatiwa na wafuasi wa upande huu kama kina Ommy Crazy na baadhi yao
Tutamatishe kwa kuangalia hizi pande tatu, Efm na Matamasha yake ni mtu anaepambana kivyake na anatengeneza base yake hanashida. Kwa Clouds na Wasafi mpaka sasa inaaminika mko kwenye marumbano makubwa, ila clouds hawajonesha majigambo yoyote wala kujibu chochote na wamebaki kudhihirisha ukomavu wao katika nyanja hiyo.
Najiuliza hivi...
Fiesta na Wasafi festival ni kitu kimoja kinachomilikiwa na mtu mmoja..?
Majigambo na Vijembe vinamalengo ya kuhadaa mashabiki na kutengeneza pesa..?
Kama si kitu kimoja Dudu Baya alitumika ili kutoa milage..?
Kama ni kitu kimoja lengo nikumdhoofisha mpinzani Efm..?
Je ni kitu kimoja ndio maana Wasafi wakapewa Ray ili afanye jingle za Wasafi festival..?
Kama sio kitu kimoja basi Wasafi mmeanza vibaya na Anguko lenu halitakuwa mbali, Kupendwa na kuwa na mashabiki wengi wanaowapenda wasanii wenu hakuwezi kwenda sawa na kupendwa kwa Kituo cha TV, Redio na Tamasha.
Ahsante.