Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kwa namna fulani matokeo tunayoambiwa ya uchaguzi kuwa CCM wamechukua viti vya Bunge kwa 100% mimi binafsi nimeyapokea kwa furaha sana, sio kwa kuwa naipenda CCM, la bali kwa kuwa CCM na wananchi kwa ujumla bado hawajatambua umuhimu wa kuwa na wabunge wa upinzani. Binafsi ningependa idadi ya viti sawa Bungeni kwa CCM na Upinzani, lakini mbunge yeyote wa upinzani akishinda kwenye uchaguzi huu ningependekeza ajiuzuru kuwapa CCM viti 100%.
Kuwa na wabunge wachache wa upinzani Bungeni ilikuwa ni kupotezeana muda tu. Michango na kauli za kitoto sana vilitawala toka pande zote mbili hadi baadhi yetu kuujiuliza kwa nini wabunge waitwe waheshimiwa!
Kwa upinzani ilikuwa mapema sana kwao kushangilia kuwa Magufuli alishindwa kuua upinzani nchini, na sasa nadhani wameelewa Magufuli alimaanisha nini! Na pia, CCM wasiwe na haraka kushangilia huu ushindi wa 100%. Kuna mambo makuu matano yanawezwa kusababishwa na CCM kuwa na 100% ya wabunge Bungeni.

- CCM sasa wanaweza kubadilisha katiba wanavyotaka, kutia ndani kumfanya Magufuli awe raisi wa maisha
- Bunge halitachukua muda mrefu kufanya vikao vyake, lakini kutakuwa na manung'uniko mengi ya wabunge kuwa wanaburuzwa
- CCM hawatakuwa na wigo wa kuwalaumu wapinzani kwa lolote linalohusu nchi hii - jimbo lisipokuwa na maendeleo hakuna tena kisingizio kwamba ni kwa sababu mlimchagua mbunge wa upinzani
- Wananchi hawahitaji tena kuambiwa au kukumbushwa mabaya ya CCM, kama kuna mabya yanafanyika kila mtu atajua ni CCM wanaosababisha
- Ugomvi na kutoelewana ndani ya CCM kutachukua hatua mpya bila kuwapo wapinzani wa kuwalaumu kwa lolote linalosababisha ugomvi ndani ya CCM kati ya wabunge na viongozi wa serikali