Ni bora nife nikifukuzana na ndoto zangu kuliko kufa njaa kwenye dunia isio na haki

Ni bora nife nikifukuzana na ndoto zangu kuliko kufa njaa kwenye dunia isio na haki

Joined
Nov 3, 2022
Posts
74
Reaction score
146
Kipi special sanaa katika hii dunia kinachoweza kunijali kwa dhati eti nikionee huruma??? Eti kinifanye nicheze kwa standards zilizo fair, hakipo, so ni muda wa kuwa ruthless.

Anaekuhubiria uache pombe, anatembea na mke wako

Anaekukamata haujalipa kodi, anapita na pesa zote za mradi wa mtaani kwako.

Nini maana ya uwepo wangu kama watoto wangu watakula mawe?
Nini maana ya legacy yangu kama nitabaki kutamani na kusengenya wengine waliofanikiwa?

Yani ulimwengu umejiandaa na makucha pale napotoka tu mlangoni, dunia imejiandaa na mapanga pale tu napokanyanga ardhini, tayari kunipigisha za uso alafu unaniambia nijipe moyo eti sijui ridiki ni mafungu, mafungu ya nini???? Ya yanya au???

kisa ww una pakumzikia pazuri unajifanya kuwa motivational speakerr unakula hela za bando za youtube huku sisi tunabaki na fikra za uongo.

hauna tabu yangu, hauna ukata wangu.

Watch this space...
 
Mkuu una tatizo la kisaikolojia linaitwa Ant-social personality disorder. Jaribu kujichanganya na watu hasa waelewa ili kupunguza ukubwa wa tatizo.

Ikishindikana kabisa anza kuhudhuria maeneo yenye watu wengi kama Club na viwanja vya mpira huku ukijaribu ku-socialize kidogo.

Mwisho tafuta demu acha kabisa punyeto.
 
Back
Top Bottom