Ni bora upange karibu na ofisi kwa kodi kubwa au upange mbali kwa gharama kubwa na usafiri wa taabu

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
345
Reaction score
1,145
Upange karibu na ofisi kwa kodi kubwa

Mfano: Upange kwa gharama X, umbali wa ofisi dakika 10

au

Uende mbali kwa nusu ya kodi ya kuwa karibu, Gharama za usafiri kubwa na usafiri ni taabu

Mfano: Upange mbali kwa nusu ya gharama X, usafiri laki 1, unaamka alfajiri kuwahi usafiri
 
Muda ni jambo la muhimu sana, kila kitu kinahitaji muda. Bora upange karibu na kazi kuliko kupanga mbali na bado hakuna unafuu wa gharama.
Kabisa mkuu. Halafu asubuhi unachokutana nacho huwa kinaboresha au kuharibu siku nzima. Sasa kama kila siku asubuhi unaanza na tabu za usafiri unaweza usiipende kazi yako.
 
Upange karibu na ofisi kwa kodi kubwa

Mfano: Upange kwa gharama X, umbali wa ofisi dakika 10

au

Uende mbali kwa nusu ya kodi ya kuwa karibu, Gharama za usafiri kubwa na usafiri ni taabu

Mfano: Upange mbali kwa nusu ya gharama X, usafiri laki 1, unaamka alfajiri kuwahi usafiri
Mkuu kwenye kichwa cha habari umesahau kumalizia "KWA WANAOISHI DAR"

Manake hiyo issue ni very specific kwa wakaaji wa mkoa huo tu hapa Tanzania.
 
Kabisa mkuu. Halafu asubuhi unachokutana nacho huwa kinaboresha au kuharibu siku nzima. Sasa kama kila siku asubuhi unaanza na tabu za usafiri unaweza usiipende kazi yako.
Inakera sana hasa kwa dar ni balaa tupu yani kabla hujafika kazini ushatokwa na jasho kwa kurupushani za usafiri.
 
Upange karibu na ofisi kwa kodi kubwa

Mfano: Upange kwa gharama X, umbali wa ofisi dakika 10

au

Uende mbali kwa nusu ya kodi ya kuwa karibu, Gharama za usafiri kubwa na usafiri ni taabu

Mfano: Upange mbali kwa nusu ya gharama X, usafiri laki 1, unaamka alfajiri kuwahi usafiri
Sehemu ili iwe mbali inatakiwa iwe kilomita ngapi kutoka kazini kwako?
 
Kuishi karibu na ofisi inakupasa usiwe na mambo mengi.

Ila ukiwa na mambo mengi , ni rahisi sana kazi kuharibika.

Hivyo option ya kukaa mbali na ofisi ni nzuri zaidi.
 
Kama unapanga nyumba nzima ni bora upange mbali kwanza ni rahisi kuilipa Kodi ya miezi sita kwa mkupuo mmoja, Fikiria Kodi ya nyumba zima ama apartment maeneo ya katikati ya jiji halafu uilipe kwa mkupuo wa miezi sita ni changamoto endapo mshahara sio mnono.
 
Back
Top Bottom