Ni bora uwe tajiri mwenye upweke au masikini usie mpweke?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
1. Uwe tajiri mwenye bilioni+ yako lakini ni mpweke, watu pekee unaoweza kuwa nao ni wale wa kununua kama bidhaa ama kujifanya wapo karibu na wewe ili wafaidi pesa zako (machawa, wapambe, gold diggers)

2. uwe n mshahara wa laki 2 lakini una marafiki na ndugu kibao wanaokujali licha ya hali yako kiuchumi
 
Sasa ukiwa tajiri si unaita tu mademu ukiwa mpweke.

Umasikini sikieni tu.
upweke unazungumziwa hapa ni kukosa watu wa kukujali kwa mioyo yao kama ulivyo.

pesa inaweza kununua hata watu lakini sio kukujali sincerly
 
Bora nikose kila kitu lkn sio pesa, bora niwe mpweke lkn pesa nnayo.
 
Mnaongea msichokijua unakuwaje na hela halafu unakuwa mpweke how?
 
Kaa na marafiki zako mi nipate hela marafiki nitawapata nikienda vacation Paris.
jaribu kuielewa maada basi, hao marafiki unaoenda kula nao bata ni wamefata pesa kuliko wewe
 
Mleta uzi acha masiahara..uwe maskini alaf usiwe mpweke. Hiv unaujua umaskini au unausikia tu, inafika muda mpka ndugu we a karibu kabisa wanakutenga.
 
upweke unazungumziwa hapa ni kukosa watu wa kukujali kwa mioyo yao kama ulivyo.

pesa inaweza kununua hata watu lakini sio kukujali sincerly
Pesa Yangu ndo Rafiki,
Pesa Yangu ndo familia
Pesa Yangu ndo security Yangu
Pesa Yangu ndo furaha Yangu
Ogopa sana wanaokuzunguka ogopa sana ni kheri mbwa Wa getini unaempa kula atakulinda kuliko binadam unaemuona muda wote anakuchekea
 
Pesa ni Mungu wa Dunia, upweke utatoka wapi? Si nitanunua marafiki? Nipeni hiyo pesa nitese ningali hai!
 
1. Uwe tajiri mwenye bilioni+ yako lakini ni mpweke, watu pekee unaoweza kuwa nao ni wale wa kununua kama bidhaa ama kujifanya wapo karibu na wewe ili wafaidi pesa zako (machawa, wapambe, gold diggers)

2. uwe n mshahara wa laki 2 lakini una marafiki na ndugu kibao wanaokujali licha ya hali yako kiuchumi
Ni bora niwe tajiri mwenye upweke na hii hali kwa sasa ndio nayoipitia kuliko umasikini wenye kudhalilisha
 
1. Uwe tajiri mwenye bilioni+ yako lakini ni mpweke, watu pekee unaoweza kuwa nao ni wale wa kununua kama bidhaa ama kujifanya wapo karibu na wewe ili wafaidi pesa zako (machawa, wapambe, gold diggers)

2. uwe n mshahara wa laki 2 lakini una marafiki na ndugu kibao wanaokujali licha ya hali yako kiuchumi
Umaskini ni ugonjwa mbaya sana sikieni tu kwa watu...
 
upweke unazungumziwa hapa ni kukosa watu wa kukujali kwa mioyo yao kama ulivyo.

pesa inaweza kununua hata watu lakini sio kukujali sincerly
Kila mtu anawatu wake loyal.

Haijalishi ana kipato au la.
 
Back
Top Bottom