Ni chakula gani ambacho ulikila unaridhika..

Ugali wa unga mahindi uliochanganywa kidogo na unga wa muhogo kwa samaki za kukaanga/dagaa na mchicha wa nazi au chuku chuku wenye nyanya chungu pembeni kuna Pilipili mbuzi/kichaa. Huwa najisikia raha sana kula chakula hiki si mchana si usiku.
Hizo nguvu za huo msosi haujawahi muacha mtu salama
 
Ugali dona..mlenda wa karanga na mtindi..daaah hua unanifanya nikumbuke kwetu somanda..
 
Ugali kwa mlenda!!! Duuh ushanitia njaa, hebu nikanunue bamia...
 
Ugali wa unga mahindi uliochanganywa kidogo na unga wa muhogo kwa samaki za kukaanga/dagaa na mchicha wa nazi au chuku chuku wenye nyanya chungu pembeni kuna Pilipili mbuzi/kichaa. Huwa najisikia raha sana kula chakula hiki si mchana si usiku.
Huu msosi tulikuwa tunafunga safari ndefu sana kuufuata mwaloni Mwanza.
 
Ugali mkubwa na ugali mdogo

Yaani huo mdogo ndo unakua mboga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…