Ni changamoto gani uliyowai kukutana nayo ulipokuwa unatafuta bidhaa yako Kariakoo?

dgombusi

Senior Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
141
Reaction score
200
Kama ndiyo mgeni umefika Kariakoo mara ya kwanza kuna kale ka hofu sijui nitatapeliwa,

Mi mara ya kwanza naenda Kariakoo nilikua natafuta simu nikawa naulizia simu kwenye duka Fulani hivi.

Jamaa alikuwa karibu nalile duka lile kama kijana wa hapo akadakia kuna chimbo simu used hadi elfu 30 tu unapata, Mimi nikaona tiyari fursa hii kumbe mimi ndiyo nilikuwa fursa, tukawa tunaongozana nae kuelekea kunako hilo chimbo.

Ile nageuka kumuaga yule mdada wa kwenye lile duka akaniita kwa ishara nikaenda akaniambia utatapeliwa mimi simjui huyo kijana kwahiyo kuwa makini au tafuta mwenyeji akutafutie.

Hapo ndipo nikakumbuka ule usemi usemao za kuambiwa changanya na maji nikapanda zangu dalala kurudi nyumbani.

Je wewe ulipata changamoto gani ulipokuwa unatafuta chimbo la bidhaa yako Kariakoo kwa mara ya kwanza.

Share nasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…