Ni changamoto ipi umekutananayo katika kuripoti

Mchochezi

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
10,962
Reaction score
7,830
Habari ndugu walimu wapya, ikiwa leo ndio siku ya kwanza ya kuripoti katika wilaya uliyopangiwa, tuambie ni changamoto au matatizo yapi umekumbana nayo wakati huu wa kuripoti? Karibuni ndugu walimu
 
Wait.. Nipo kwenye semina ya pspf ntakujuza bdaye!!
 
Kuna issue ya Medical Examination form, unalipia 2000/= ila sahau kuhusu risiti.
 
ntakwambia baadae nipo nachukua fedha ya kujikimu
 
Matumiz jaman vihela hvyo mishahara huwa inachelewa kuanza.
 
Kuna issue ya Medical Examination form, unalipia 2000/= ila sahau kuhusu risiti.

Hiyo ni ndogo! Sumbawanga ni 5000, risiti zipo, vipimo hakuna (daktari anapima kwa macho).
Kimsingi, Halmashauri ya Sumbawanga V hawakujiandaa vizuri kupokea watumishi wapya.
Hapo awali alianza kwa kukagua vyeti vya elimu. Zoezi hilo lilisitishwa mapema sana, hata waalimu kama 20 kati ya wote, hawakukaguliwa.
Baada ya hapo, saa tano kasoro, maafisa walikuwa katika vikundi vikundi wakijadiliana (ikionekana kana kwamba hawajui cha kufanya).
Ilipofika saa tano na dakika kadhaa, zilianza semina kutoka benki, mifuko ya pensheni, maafisa mbalimbali wanaoshughulika na Elimu.
Kulikuwa na mkanganyiko wa maelezo kutoka kwa watoa mada. Kwa mfano, CRDB, NBC na NMB juu ya benki inayokuwa ya kwanza kupokea mshahara. Pia, mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya alisema kwamba kujiunga au kujitoa CWT ni hiari (CWT ni chama cha hiari). Ili hali mwakilishi wa CWT alisema kujiunga ni hiari, kukatwa ni lazima kwa CWT inatetea maslahi ya waalimu wote.
Zoezi hilo lilikamilika takribani saa nane kasoro. Baada ya hapo mchakato wa ukaguzi wa vyeti uliendelea, ....
Hakuna mwalimu aliyefanikiwa kujaza mikataba ya ajira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…