Ni changamoto ipi umekutananayo katika kuripoti

Ni changamoto ipi umekutananayo katika kuripoti

mambo ya kupambana na chaki aisee na vumbi lote lile, nifundishe wanafunzi 200 darasa moja, nisahihishe madaftari yote yale, niwahi shule saa moja, niondoke saa kumi na moja, usafiri kufuata mshahara nako ni gharama sawa na robo mshahara.... negatives ni nyiiingi kuliko positives! dah...

nikiwaza hapo mi huwa moyo unaenda mbio na kupoa ghafla!!
 
Hiyo ni ndogo! Sumbawanga ni 5000, risiti zipo, vipimo hakuna (daktari anapima kwa macho).
Kimsingi, Halmashauri ya Sumbawanga V hawakujiandaa vizuri kupokea watumishi wapya.
Hapo awali alianza kwa kukagua vyeti vya elimu. Zoezi hilo lilisitishwa mapema sana, hata waalimu kama 20 kati ya wote, hawakukaguliwa.
Baada ya hapo, saa tano kasoro, maafisa walikuwa katika vikundi vikundi wakijadiliana (ikionekana kana kwamba hawajui cha kufanya).
Ilipofika saa tano na dakika kadhaa, zilianza semina kutoka benki, mifuko ya pensheni, maafisa mbalimbali wanaoshughulika na Elimu.
Kulikuwa na mkanganyiko wa maelezo kutoka kwa watoa mada. Kwa mfano, CRDB, NBC na NMB juu ya benki inayokuwa ya kwanza kupokea mshahara. Pia, mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya alisema kwamba kujiunga au kujitoa CWT ni hiari (CWT ni chama cha hiari). Ili hali mwakilishi wa CWT alisema kujiunga ni hiari, kukatwa ni lazima kwa CWT inatetea maslahi ya waalimu wote.
Zoezi hilo lilikamilika takribani saa nane kasoro. Baada ya hapo mchakato wa ukaguzi wa vyeti uliendelea, ....
Hakuna mwalimu aliyefanikiwa kujaza mikataba ya ajira.

pole sana mkuu
 
mambo ya kupambana na chaki aisee na vumbi lote lile, nifundishe wanafunzi 200 darasa moja, nisahihishe madaftari yote yale, niwahi shule saa moja, niondoke saa kumi na moja, usafiri kufuata mshahara nako ni gharama sawa na robo mshahara.... negatives ni nyiiingi kuliko positives! dah...

nikiwaza hapo mi huwa moyo unaenda mbio na kupoa ghafla!!

na wewe ni mwl mpya au?
 
Huku benki ni moja tu...ile ya 'makabwela,'
huna akaunti...fomu zipo unajaza, unafungua...

Sijasikia, wala sijui chochote mpaka dakika hii niandikapo kuhusu CWT

...Ilipofika saa tano na dakika kadhaa, zilianza semina kutoka benki...Kwa mfano, CRDB, NBC na NMB...
 
Pigeni kazi wakuu ila kama mlikuwa mumezoea town? Daah I'm real sorry kwa kuwakosa JF hadi likizo
 
Back
Top Bottom