Kuhusu maji nilivuta kwa gharama zangu(laki mbili) mwanzoni kabisa wakati nafanya ukarabati wa location, niliunganisha bomba kwenye simtank la lita 1000 ambapo maji yanaenda kwenye simtank halafu mashine ya water pressure naiunganishia kutoka kwenye simtank maji yalikuwepo ya kutosha sikuwahi kupata changamoto.
Umeme nilikuwa nachangia na wengine ila niliweka meter ya kusoma unit ninazotumia mimi peke angu., gharama za uendeshaji nilikuwa nazitenga kwa siku maana kukaa na hela mwezi mzima hapo kati unaweza kutumia kwa mambo mengine halafu ukija muda wa kulipa bills hela haipo.
Kila siku natenga 20k pembeni ambapo maji 5000, umeme 5000, sabuni na spray 4000. Hizo gharama zote hazibaki hivyo hivyo kila siku mfano maji kwa siku naweza kutumia ya 3000 tu, au spray naweza kununua ya elfu 10 nikatumia hata wiki nzima kwahiyo nilikuwa naweka gharama kima cha juu kidogo maana bora hela ibaki kila kitu kikiwa kimefanyika kuliko iishe huku mengine hayajafanyika.
Vile vile nilikuwa natenga 1000 kila siku kwa ajira ya ulinzi na 5000 ya kodi(nilikua nalipa 150k/month kwaiyo 5000×30=150k). Haikua car wash ya hadhi ya juu naweza kusema ni ya hadhi ya chini kuelekea hadhi ya kati. Siku ambayo biashara haikua nzuri nilikua nalaza 20k baada ya kutoa costs zote kuna siku ambazo nilikuwa nalaza mpaka 50k sana sana siku za wikiendi.
Matarajio yangu yalikuwa mengi ikiwemo kuongeza mashine ili nihudumie magari mengi kwa pamoja na kuongeza eneo ili niweze kuhudumia mpaka magari makubwa kama mabasi ya mikoani ni mpaka pale mgao wa umeme ulipoanza biashara ikawa inasuasua umeme unakatika saa 2 asubuhi unarudi saa 1 usiku, nikalazimika kufunga biashara.
Kwahiyo kwa upande wangu changamoto iliyoniangusha ni mgao wa umeme.