JF Doctors,
mimi nina tatizo, kila ninapoenda haja ndogo (kukojoa) hufuatia maumivu yenye kuashilia kama sijamaliza kukojoa, baada ya muda kidogo nikienda kukojoa kwa kukamua hutoka mkojo kidogo na hapo ndipo hupata nafuu kidogo. Je! Hii ni maradhi gani?
Kutokana na maelezo yako japo kuwa sio timilifu
yani hayajitoshelezi inaonyesha unaweza kuwa na moja kati ya hivi vitatu
MOJA: UTI, urinary tract infection
PILI: stone
Tatu,BPH lakini hii ya tatu labda kama unakojoa mara nyingi kwa mda mfupi na mkojo unaokojoa unakuwa kidogo
inaitwa Benign Prostate Hyperplasia so nenda kwa Urologist akakuangalie utakuwa na jibu.
Mara ya mwisho ulikutana kimwili lini? Wakati mwingine inawezekana kukawa na ka mchumbuko kidogo kwenye mfereji wa njia ya mkojo kutokana na matumizi ya kiungo chako au kama hujatumika siku nyingi basi hiyo itakuwa ni maambuzikizi ya bacteria ( bacteria infection) , inawezekana Njia ya Mkojo imeathirika kidogo Mkuu. Tumia anti-biotic kama Aziwok au Ciprofloxacin uangalie maendeleo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.