Ni dalili ya uchawi au kawaida?

Ni dalili ya uchawi au kawaida?

Habarini za humu JF,

Mimi ni kijana wa umri miaka 27. Ninafanya kazi katika company flani hivi. Nataka niulize je hii ni dalili ya kuwa mchawi au lah?

Kutokana na katabia ka kuona wivu maendele ya watu naumia moyoni na ninakuwa na mawazo pia. Leo kuna mtu ninafanya nae kazi kaniambia anataka kununua gari, basi nimekuwa sina raha nae moyo wangu umejikunja sana mimi kimaisha nimemzidi ila akinunua gari atakuwa juu yangu.

Je, hii ni kawaida au ndo naanza kuwa na roho chafu, binafsi sipendi kumchukia mtu au kumuona katika hali mbaya ila akifanifikiwa roho inauma.

Nawasilisha..
Kwanza ww ni kabila gani mkuu!! Kuna vitabia huwa ni asili yaani inbone character/traits .
 
Kuwa mchawi SI kweli ila hiyo roho inaweza kusukuma ukafanya ubaya
Wivu ni kawaida na kama huna wivu hutafanikiwa lakini usiwe wivu WA kutaka kuwangamiza wengine Bali wivu WA kusukuma Zaid katika mafanikio. Unapopatwa na Hali hiyo mbariki mhusika moyoni mwako na kumsukuru Mungy kwa ajili ya mafanikio yake, huku nawe ukimwomba Mungu akubarikitaratibu utaona utaanza kufurahia mafanikio ya wenzako huku na wewe ulifanikiwaa.
Halafu mafanikio ni package kubwa sana sio vitu tu pekee Kuna amani ya moyo, mahusiono mema , afya na uwezo WA kupata mahitaji yako ya muhimu.
 
Shukrani mkuu
 
Pole sana. Binafsi naona hiyo ni aina flani ya ubinafsi. Nachojua ungeanza wewe kununua gari alafu akaja kukwambia anataka kununua nayeye, usingeumia kiasi hicho. Alafu ndugu yangu, Mungu humpa kila mtu riziki yake na kwa wakati wake. Amini usiamini, mshahara wako mnono kumzidi, haina maana utamzidi kila kitu.
 
Nikajua utataka muongozo ili uache hiyo hali.. kumbe unataka ujue tu kama upo kwenye uchawi au laah.. MKUU andika uzi mzuri jinsi gani utaweza kuondokana na hiyo hali tuje kukupa muongozo kuondokana nayo inawezekana na rahisi tu kwa kuwa haujataka/haujaomba muongozo kuondokana na hiyo hali ngoja tukuache.. pole mkuu stage mbaya sana hiyo katika maisha ya mwanaadamu.. polee
 
Utafiti unaonyesha kila binadamu ana ka ubinafsi alikozaliwa nako so kawaida sana ila kasipitilize sio ww tu hata hao wanaokupinga hapa juu[emoji121][emoji121][emoji121] nao ni hivyo ila mtu huwezi kujieleza jins ulivyo kwa sifa mbaya utajielezea kwa mazuri
 
Usiwe unafuatilia shughul za wengine, ,kufuatilia taarifa za watu wengine ndiyo unakutana na habari za Maendeleo ya watu wako wa karibu hivyo kiasili ni lazima moyo ushtuke, na shetani akishajua huwa unashtuka sababu ya mambo yasiyokuhusu atakuletea watu wanaozungumzia habari za Maendeleo ya watu wengine ili uchukie vizuri. Mwisho wa siku unasema roho inakuuma kumbe ni wivu umekujaa. Halafu haya mambo yanafanyika kwenye nafsi lakini madhara yake yatakaa na wewe na usijue tatizo ni nini.
 
Acha Tabia Za Police, Utauwa Watu Kama Police Wa Mtwara Bure
Yatakutokea Puani
Sijui kama ni kila askari ana tabia za hao polisi..... ASKARI NI MUHIMU SANA KWA JAMII HASA UKISHAJUA.. Wla usitumie tena mifano kama hii.
 
Nmecheka kama mazuri [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]..
Sema nini Braza " usipokua na malengo utaingia sana mwenye malengo ya watu wengine"

Yani wewe utaingia sana mwenye malengo ya watu kwasababu ya roho yako! Panga malengo yako ili malengo ya watu yasikusumbue La sivyo utakua unafanya kila anachofanya mtu mwingine ili roho itulie
Kama malengo yako Nyumba tembea humo achana na gari

I am taking this…
 
Usiwe unafuatilia shughul za wengine, ,kufuatilia taarifa za watu wengine ndiyo unakutana na habari za Maendeleo ya watu wako wa karibu hivyo kiasili ni lazima moyo ushtuke, na shetani akishajua huwa unashtuka sababu ya mambo yasiyokuhusu atakuletea watu wanaozungumzia habari za Maendeleo ya watu wengine ili uchukie vizuri. Mwisho wa siku unasema roho inakuuma kumbe ni wivu umekujaa. Halafu haya mambo yanafanyika kwenye nafsi lakini madhara yake yatakaa na wewe na usijue tatizo ni nini.

Huyu alinifata mwenyewe kuniambia
 
Mimi mwenyewe niko hivo hivo ,nikiona rafiki zangu wametusua maisha mazuri ,nakuwa na hasira kinoma ,wanakuwa kama maadui kwangu aisee..[emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom