DOKEZO Ni dhahiri kabisa TTCL inahujumiwa, Meneja Masoko TTCL achunguzwe ikibidi afukuzwe kazi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ni dhahiri kabisa TTCL inahujumiwa meneja masoko TTCL achunguzwe ikibidi afukuzwe kazi!

Hili shirika ni dhahiri linahujumiwa kwa maksudi, ni aibu kwa shirika kama hili ambalo linatumia mabilioni ya walipa kodi kusimika mitambo nchi nzima halafu kuwepo kwa mambo ya ajabu hivi.

Hivi mnajua kuwa TTCL ndo mtandao ghali zaidi Tanzania kwa sasa? Wakati wenzao wanauza gb kwa 1200 hadi 1300 wao wanauza gb kwa 1600.

Vifurushi vyao ni ghali sana, sio dakika sio sms, hawa walitakiwa wawe na unafuu kidogo ili watu watumie kwa wingi then mapato yapatikane.

Nasema haya kwasababu, Serikali imetumia mabilioni ya pesa kulilifua hili shirika lakini wayafanyayo hayastahili kabisa.

Halafu pamoja na kuenea karibu nchi nzima, meneja masoko hana mpango wowote wa kufanya promo kama yafanyavyo makampuni mengine.

Yeye yupo kwa maslah ya wengine nadhani, pale ttcl kulikua na mchezo wa meneja kupokea mishahara miwili, mmoja analipwa na ttcl/serikali mwingine anaingiziwa na hizi kampuni shindani.

Kifurushi cha bufee kiliwafanya hawa jamaa kujizolea mamia ya watu sasa hivi wamekiharibu kiukweli huyu meneja wa masoko hafai kabisa kuendelea kuwepo pale, anatumika kuua shirika.

Tukiendelea kuchekea huu upuuzi tutajuta siku moja tunapoteza mabilioni ya pesa kufufua mashirika kama haya halafu kikundi cha watu wachache kinaua shirika kwa mgongo wa nyuma kupitia hawa makanjanja wanaofanya kazi shirikani.

Meneja masoko TTCL asimamishwe kazi, mkurugenzi naye abadilishwe, hili shirika bila hivyo linaenda kufa tena!
Nadhani hili la Mkurugenzi lilifanyiwa kazi.
La meneja masoko sijui.

Halafu "sala" zako zilitakiwa zilenge kuanzia uozo unapoanzia, ungeanzia kwa Waziri wa mawasiliano, naye pia hafai na siyo msaada kwetu.

Huyu ndiye amekuwa ni mwiba wa kupanda kwa bando na data maana anawalinda na kuwakingia kifua makampuni ya simu!

Aliahidi mwezi wa kwanza 2023 bei za vifurushi zitatizamwa upya, mpaka tunaumaliza mwezi, hilo limefanyika?

Tushaonekana waTz maboya sana, kama raia hatuna uwezo wa kupaza sauti zetu popote zikasikilizwa!

Lakini yote haya kwakuwa yana mwanzo, pia mwisho upo.
 
Ni dhahiri kabisa TTCL inahujumiwa meneja masoko TTCL achunguzwe ikibidi afukuzwe kazi!

Hili shirika ni dhahiri linahujumiwa kwa maksudi, ni aibu kwa shirika kama hili ambalo linatumia mabilioni ya walipa kodi kusimika mitambo nchi nzima halafu kuwepo kwa mambo ya ajabu hivi.

Hivi mnajua kuwa TTCL ndo mtandao ghali zaidi Tanzania kwa sasa? Wakati wenzao wanauza gb kwa 1200 hadi 1300 wao wanauza gb kwa 1600.

Vifurushi vyao ni ghali sana, sio dakika sio sms, hawa walitakiwa wawe na unafuu kidogo ili watu watumie kwa wingi then mapato yapatikane.

Nasema haya kwasababu, Serikali imetumia mabilioni ya pesa kulilifua hili shirika lakini wayafanyayo hayastahili kabisa.

Halafu pamoja na kuenea karibu nchi nzima, meneja masoko hana mpango wowote wa kufanya promo kama yafanyavyo makampuni mengine.

Yeye yupo kwa maslah ya wengine nadhani, pale ttcl kulikua na mchezo wa meneja kupokea mishahara miwili, mmoja analipwa na ttcl/serikali mwingine anaingiziwa na hizi kampuni shindani.

Kifurushi cha bufee kiliwafanya hawa jamaa kujizolea mamia ya watu sasa hivi wamekiharibu kiukweli huyu meneja wa masoko hafai kabisa kuendelea kuwepo pale, anatumika kuua shirika.

Tukiendelea kuchekea huu upuuzi tutajuta siku moja tunapoteza mabilioni ya pesa kufufua mashirika kama haya halafu kikundi cha watu wachache kinaua shirika kwa mgongo wa nyuma kupitia hawa makanjanja wanaofanya kazi shirikani.

Meneja masoko TTCL asimamishwe kazi, mkurugenzi naye abadilishwe, hili shirika bila hivyo linaenda kufa tena!
Sema wewe mwamba utakuwa unafanya kazi humo ndani
 
Hatimaye yanatimia kweli yasemwayo humu JF yapo na kama hayapo yanakuja
 
Back
Top Bottom