DOKEZO Ni dhahiri kabisa TTCL inahujumiwa, Meneja Masoko TTCL achunguzwe ikibidi afukuzwe kazi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Nadhani hili la Mkurugenzi lilifanyiwa kazi.
La meneja masoko sijui.

Halafu "sala" zako zilitakiwa zilenge kuanzia uozo unapoanzia, ungeanzia kwa Waziri wa mawasiliano, naye pia hafai na siyo msaada kwetu.

Huyu ndiye amekuwa ni mwiba wa kupanda kwa bando na data maana anawalinda na kuwakingia kifua makampuni ya simu!

Aliahidi mwezi wa kwanza 2023 bei za vifurushi zitatizamwa upya, mpaka tunaumaliza mwezi, hilo limefanyika?

Tushaonekana waTz maboya sana, kama raia hatuna uwezo wa kupaza sauti zetu popote zikasikilizwa!

Lakini yote haya kwakuwa yana mwanzo, pia mwisho upo.
 
Sema wewe mwamba utakuwa unafanya kazi humo ndani
 
Hatimaye yanatimia kweli yasemwayo humu JF yapo na kama hayapo yanakuja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…