Ni dhahiri kuna kila dalili ya goli la mkono katika uchaguzi wa mwenyekiti CHADEMA hapo January

Ni dhahiri kuna kila dalili ya goli la mkono katika uchaguzi wa mwenyekiti CHADEMA hapo January

Subira the princess

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2018
Posts
3,474
Reaction score
3,744
Wasalaam

Wote tumeshuhudia bwana Freeman Mbowe akiapa kushinda uchaguzi inyeshe mvua au liwake jua.

Ukiangalia nguvu za kiuchumi za huyo mheshimiwa ni kwamba atatumia rasilimali zake kushawishi wajumbe wa kamati kuu kumchagua kwa kura za kishindo.

Ukija upande wa pili mh Lissu amelalamika mara kadha kuwepo kwa rushwa ktk chaguzi za kanda. Lissu anakubalika kwa hoja na idadi kubwa ya wajumbe ila hawezi kushinda uchaguzi hata akipigiwa kura na wajumbe wote ndo hapo tunasema lazima kutakuwa na goli la mkono ukizingatia uhusiano mwema uliopo kati CCM na bwana Mbowe.

Muda ni rafiki wa kweli utaongea.
 
Ikitokea hivyo CCM watakuwa.wamefauli.mkakati.wao wa kukiua chama cha chadema na kushinda uchaguzi mkuu ujao 2025 maana Chadema lazima kiparaghanyike na kukosa imani na watu tena.Tundu lisu na wanaomuunga mkono kwa vyovyote vile watatafuta uungwaji mkono kwenye chama kingine chenye ushawishi karibu na CDM.
 
Back
Top Bottom