Ni dhambi kuvaa barakoa kwa kipindi hiki?

Ni dhambi kuvaa barakoa kwa kipindi hiki?

rodian

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2016
Posts
246
Reaction score
323
Habari wakuu,

Nadhani ni muda mrefu tangu nipost last thread. Nashukuru Mungu ni mzima wa afya na kutokana na majukumu ya hapa na pale, nikashindwa ku-post, naamini hakijaaribika kitu kwani pamoja na yote nimekuwa nikipata nafasi za kusoma thread za wanajamii wenzangu,🙂 ingawa ntaimiss free basics, vimeumana, haipo kwa sasa.

Wakuu nirudi kwenye maada yangu na kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza. Nimekuwa kwenye changamoto baada ya kuanza kuvaa barakoa, yaani Watanzania wenzangu hawapendi nikivaa, iwe kwenye daladala, mtaani au nikiwa sehemu ya majukumu yangu, au ukitatisha tu sehemu lazima wakuite na waanze kukuhoji kama Corona ipo na utalazimishwa kuivua.

Je, nauliza, kuvaa barakoa ni dhambi? Kazi ambayo ninayo kwa muda huu inanilazimu nivae. Kwa mfano, Posta pale ukiingia kwenye shule au baadhi ya ofisi lazima uvae barakoa.

Naomba majibu Wakuu.

Nawasilisha.
 
Dhambi ni kutokufuata zile amri kumi za Mungu. Ya wanadamu waachie wenyewe.
 
Vaa wewe ili kulinda afya yako kila mtu na maisha yake bana! Why ujistukie kisa mtu mwingine anakuangaliaje? Mbona mama yetu nae anavaa Barakoa mda wote vaa wewe acha mchezo na maisha.
 
Back
Top Bottom