Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kwa umri wa CCM kama chama , na kwa umri wa wanachama wake na viongozi wote wazee waliopita hapo , na kwa umri ambao chama hiki kimetawala na kuongoza Tanzania ni jambo la Aibu kubwa sana ya kufunika uso kuiogopa Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi .
Uchunguzi unaonyesha kwamba viongozi wa ccm wakisikia jambo hili la Katiba mpya wanapigwa na baridi kali kiasi cha kutetemeka mwili as If ni Watuhumiwa wanaosubiri kunyongwa huku kitanzi cha kuwaning'iza kikiwa kinateremshwa kwenye shingo zao .
Labda kwa faida ya ccm , viongozi wake , wazee wao pamoja na wote waliopita hapo ni kwamba KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI havikwepeki kwa sasa , hakuna namna yoyote ile ya kulikwepa jambo hili , NO WAY ! kwahiyo jambo la msingi kwa watu hawa ni kujiandaa na kujipanga kuishi ndani ya maisha mapya yaliyojaa haki za kikatiba , habari za Akina Mahera , Jecha au Augustino Ramadhan zinakomea hapa , Mwisho wa kubebwa na hao makada wenu wanaoitwa Wakurugenzi akina Kagurumujuli , Mwakabibi na wenzao imekwisha , NOTHING LASTS LONGER , umefika wakati wa kujieleza mbele za umma mlichokifanya kwa miaka lukuki iliyopita bila kumung'unya maneno , Hakutakuwa na cha Mswalie mtume
Jifunzeni kuishi kwa haki , jifunzeni kushinda chaguzi kwa haki na kikubwa zaidi jifunzeni kuvumilia maumivu waliyoyavumilia wenzenu , Rais Mstaafu Jakaya Kikwete , aliwahi kuwaambieni kwenye vikao vyenu kwamba kama wapinzani wakisema ccm haijafanya kitu , basi ni kazi yenu kuwaambia wananchi kwamba mmefanya hiki na kile , halafu wananchi wapime wenyewe , Waonyesheni MAVIEITE na Maflyover , MADARAKA NI DHAMANA YA MUDA MFUPI TU , muda wenu umekwisha