Ni forex tena, zamu hii pokeeni ukweli huu..

Mwandiko wa Ontario huu, tumekumiss hapa Jf kila siku ID mpya tulia ujibu shutuma vizuri umejibu kwa wepesi na methali nyingi.
Ila mada imeeleweka.
Mkuu wala Ontario hahusiki hapa. Labda na yeye anasoma tu kama wengine
 
Mleta mada kama hajui namna ya kumtambua fake forex broker na anajiita amehitimu training ya forex hii ni aibu ya kiwango cha lami. Kujua broker bora ni basic knowledge kwa trader yoyote mwenye kuijua forex.


Kuanzia kichwa cha habari mpaka uzi mzima sijaona mahali popote umejbu walau hoja moja ya kashfa anazotupiwa huyo Jp Markets.


Kwa aina ya forex trader kama ya mleta mada sishangai kuona kila siku watu wanalia na kusema forex ni utapeli.
 


Just to alert you .. Matangazo mengi mengi ya mitandao ya simu ni wizi... Wanatumia kila njia wakuchomoe sh 100 au 200 ktk tangazo wanalotaka ujiunge.. Sometimes unakuta kama tigo wanakuunga ktk huduma hata hujajiunga ww then wanaanza deduction zao monthly kama 200 hv bila ww kujua, multiply watu 1 mil tu utajua wanaiba kiasi gani. Likewise Forex mnatumia uelewa mdogo wa watu kuwaibia kiaina tht is what a scammer does..!!

Kama ulikuwa hujui pia utapeli wa kimtandao hasa ktk mitandao ya simu kutumia data kuibia wateja thru MBs ukiacha huduma za kujiunga bila kujua za sms ni mkubwa sana au hiyo Forex ni mwingi sana sana, biashara kuwa halali haimaanishi hakuna scammers, wapo, na kukosa uaminifu na kuanza kuwadokolea wateja fedha zao bila wao kujua ni scamming, so acha kutumia nguvu hivyo kuaminisha watu TMT au JP ni exceptional, you are all under the same trend, wizi wa kiaina bila wateja kushtuka.. Labda nyie mnafanya wizi kidogo kidogo baadae mtaongeza.. Na kwanini [HASHTAG]#Ontario[/HASHTAG] uje na ID nyingine humu?
 
Kazingua sana huyu jamaa kaandika bandiko lefu kinoma halafu ndani umejaa utumbo m***ck
 
Sasa kumbe na wewe bure tu? Kama unajua kuna huo utapeli kwenye simu kwa nini usipige kelele uone ni kawaida wakati wengine wakipromot kazi zao ndio uone utapeli? Tuliza mpira mkuu
 
Sasa kumbe na wewe bure tu? Kama unajua kuna huo utapeli kwenye simu kwa nini usipige kelele uone ni kawaida wakati wengine wakipromot kazi zao ndio uone utapeli? Tuliza mpira mkuu

Did you know how we strictly squeezed TCRA na mchezo huo wa makampuni ya simu umekoma kwa 90%..? Au ulijua watu kama mm ni wa kutulia ? Once nikiwa na concrete evidence there is NO WAY UTAPONA.. Why? Sbb jua ukiwa na ushahidi wa kutosha hata mmoja tu wa kampuni ya simu kukuibia mfano, ukawashtaki utalipwa millions sbb sio mtu mmoja tu watakuwa walimchezea huo mchezo, compensation ni kubwa utalipwa kuwa mfano. Most internet businesses scamming ndio njia kubwa ya kujipatia fedha za haraka haraka na kuwaibia wateja, huo ndio ukweli
 
Clap Clap Clap... Sasa unangoja nini kwenda kupeleka mashitaka ya hao scammer wengine?
 
Clap Clap Clap... Sasa unangoja nini kwenda kupeleka mashitaka ya hao scammer wengine?


Time is coming... you will tell me..!! Kikubwa as i stated ni concrete evidences, then legal and illegal procedures will follow...!! Kikubwa ni kufanya business halali na kutofanya scamming ktk hizo businesses.. Bahati nzuri watu tukikaa kimya sio kwamba hatujui, tunajua sana but we are waiting certain stage ili upate kila kitu to take action..
 
Mkuu siungekuja tu na ile id yako pendwa?
 
Dah! Niseme tu sioni kipya kwenye kauli zako. Mimi hapa nasema na ninawataarifu wadau kuwa TMT wanaendelea na kozi yao fupi pale Jangid Plaza, Oysterbay. Tarehe 24 kutakuwa na classes so unaweza kuja kupata fundamentals za forex. Kingine ni mentorship ya lifetime, ila kama itafika wakati ukaona unaweza kusimama kwa miguu yako mwenyewe unaruhusiwa kuaga na kwenda kuwa independent trader.

Unajua, kelele zimeanza baada ya watu kufunguliwa macho kuhusu forex. Wamepata kuijua japo kwa msingi na wakaona waondoke. Wengine wakajiongeza kujua zaidi kuhusu forex na brokers. Wakaona baadhi ya mapungufu ndani ya TMT. Bahati mbaya hawakutumia njia sahihi kuwasilisha malalamiko yao. Wakajaa ujuaji na wengine wakafukuzwa. Ndio hao wanaitukana kila leo. Au na wewe ni mmoja wapo? Hakuna ambacho kinakosa kasoro ndugu. Ujue tu hivyo. Bahati nzuri kasoro zinafanyiwa kazi. Endelea kukusanya ushahidi na vielelezo vyako
 

Naomba nikuulize mambo machache kwenye hizi porojo zako ulizoandika hapa

1. Unapozungumzia kuumia unazungumzia kuumia kupi? Maani ni kweli hakuna broker mwenye 5 star. Lakini baadi ya complaints za clients kuhusu broker fulani huwa ni kwasababu clients wenyewe wameviolate T & C's , na ndio maana kuna baadhi ya brokers huwa wanajitokeza katika hizo reviews kujibu malalamiko ya wateja wao. Kuumia nilikozungumza mm ilikuwa ni sababu ya TMT na hiyo IB yao. Inaonekana ni wazi hujui kwamba IB ni conflict of interest kati ya Client na tutor wake.

2. Nilienda TMT nikiwa Tayari najua kuanalyse market na nikiwa najua kutrade. And I can show you my my trading history kabla hata ya hizo training kuanza maana data zipo. hakuna sehemu nimeandika kwamba mimi nilikimbilia somewhere ambako walinipa link ili na mm nikakamate vichwa vyangu na sijui hilo wewe umelitoa wapi.

3. Halafu naomba nikuulize kitu, hivi mtu akiongea ukweli anakuwa anatukana? Nowadays ukweli umekuwa matusi eh?


5.Mwisho naomba tu niseme kwamba siwezi kurudi TMT na wala hata sijawahi kutaka kujua nini kinaendelea huko baada ya kutolewa. Maana niliwaona wapuuzi tu.

Halafu swali langu la kwamba JP markets ni good broker au bad broker hujanipa majibu bado
 
TMT walituletea JP Markets. Tunawajua TMT na ofisi zao tunazijua. Kwa tatizo lolote ofisi zao ziko wazi, hivyo hakuna namna yoyote unaweza kufanya miamala yako na broker akashindwa kukulipa halali yako wakati TMT tuko nao.

Hii statement umeandika Only kwa sababu hauijui vizuri sheria ya Contracts ilivokaa. Labda kwa kukusaidia naomba ukatafute Law Of Contract Act CAP 345 R.E 2002. Kasome vizuri Parties as an important element in a contract. Then uje unijibu kwamba TMT anaingiaje kwenye contract yako ww na JP markets?
 
Naomba nikujibu kwa mkupuo kama ifuatavyo

Mosi; suala la IB na tutor ni kweli lina conflict of interest kama broker ni market maker. Kama sio basi hata trader akiunguza hela zinaingia moja kwa moja sokoni na si kwa market maker. Hii pia haizuii broker kuwa na namna zake za kupata sehemu ya hizo hela zinazoingia sokoni. Ninajua pia kuwa brokers wana access na baadhi ya setup za platform wanazotumia, kama mt4. Kwa muktadha huo hakuna aliyesalimika %100 bila kujalisha ni broker toka wapi. Ndio maana unasisitiziwa kuwa na risk management na kuchunga sana margin call.

Pili; ishu ya contract sitaki kuingia sana ila mimi ni third party kati ya hawa watu wawili. Kwa lugha nyingine mimi ni mdau. Nasema hivyo kwa maana CEO mwenyewe wa JP Markets amejoin grupu letu/zetu kuja kutoa ufafanuzi ambao tulihitaji kujua. Japo umesema contract ni kati ya JP na TMT umeona sasa nasi tumehusika. Bila clients hakuna huyo JP au yeyote yule.

Tatu umeuliza kuhusu JP markets. Hana tatizo. Wewe unazungumzia conflict kati ya IB na client. Nakwambia pia kuna conflicts nyingi kwenye makampuni na mashirika kati ya management na surbodinates (staff cadre), so sioni ajabu ya hiyo conflict unayoizungumzia wewe. La msingi client ajue anapata nini. Asipopata apaze sauti, na kwa staha. Akiona hasikilizwi hajafungwa kamba. Ila ndio isiwe tiketi ya matusi
 

1. Conflict of interest is just conflict of Interest no matter ni aina gani ya broker
2. It seems like haufahamu jinsi market maker brokers wanamake hela.
3. Inaonekana ni wazi hauijui flow ya money kuanzia kwenye Interbank mpaka inamkuta Retail trader.
4. Unaposema brokers wana access na setup za platform mfano ni setup zipi? Na wao kuwa na hiyo access how is it going to affect you?


1. Yaani contract umeingia ww na Jp markets, halafu ww uwe Third party tena?
2. Hakuna sehemu nimetaja contract kati ya Jp markets na TMT
3. CEO kuwa ndani ya Group is not a big deal na ni kwa sababu nyinyi ni clients wake.
4. Swali lilikuwa kama leo hii umezuka mgogoro let say Jp markets wamekataa kuwalipa hela. Mkaamua kufungua Kesi mahakamani maana migogoro ndio inayowapeleka watu mahakamani. Kesi yoyote lazima iwe na parties wawili, Part ya kwanza ni ww na part ya pili ni Jp markets. Now tell me TMT anaingia wapi?
 
Reactions: 911
Unajua, wakati forex inakuwa introduced hapa hatukuwa tunamjua broker yoyote [wengi wetu]. Sasa alipokuja TMT na ambaye ni IB alifanya hayo kwa niaba yetu. Tulijiunga na JP kwa kupitia TMT ambaye anatoa mafunzo pamoja na maelekezo mengine. Kwa lugha nyingine TMT wanahusika sana kuprotect interests za clients kwani hata deposits zingine zinapitia pale. Ikifika wakati ukawa independent trader si lazima kuwa chini ya TMT. Unaweza kuwatafuta mwenyewe kwa njia zako ukadeposit, ukatrade na kuwithdraw. Hapo TMT hawahusiki kwa vyovyote. Kwa utaratibu wa sasa TMT wako liable kwa lolote litakalotokea. Hii naona iko sawa maana TMT iko registered hapa bongo. Ila pia ikifika wakati na wao wakawa broker, itapendeza zaidi kwa kuwa tunawajua
 
Wabongo kwa majungu bwana utasema tumelogwa! Ontario ana make money nyie kazi kubwabwaja tu. Tudownload pesa bwana na tutafute skills zaidi za kudownload hela hapa mjini. Mtaongea na kufungua nyuzi kibao za ontario lakini yeye anawachora tu maana mtaishia kusemasema tu halafu hakuna kinachoendelea! KAMA KWELI MMEONA UMUHIMU WA FOREX KATIKA MAISHA YENU KWA NINI MSIACHANE NA ONTARIO MKAPIGA ZENU PESA!? TUFANYE KAZI YA KUDOWNLOAD BWANA NA KWA WALE MAGWIJI FUNGUANI NYUZI ZA KUELEMISHANA ZAIDI SIYO HIZI ZA MAJUNGU YA KISWAHILI SWAHILI!
 
Hujausoma uzi wewe. Tatizo unasoma tu vichwa vya habari na kukimbilia kuandika. Sio nzuri kiafya
 
Kwa wale Trader ambao wangependa kumtumia broker Templerfx.

Broker huyu anakuwezesha kuweka PESA na kutoa kwa njia ya M-PESA.

Kujisajili ni rahisi sana kwa kutumia kitambulisho chako cha kupigia kura na namba yako ya simu utakayotumia kuweka na kutoa pesa kwa broker.

JISAJILI SASA
Usisite kuomba msaada

TemplerFX | Promo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…