Nataka kununua gari ya kutumia lakini napata taabu kidogo kujua ni gari ya aina gani itanifaa kwa kuzingatia kwamba napenda gari ambayo haizidi cc 2400, iwe na 4 wheel, wenyewe wanita SUV, nimejaribu kuangalia na kuvutiwa na Toyota liteace noah, Nissan Serena, Mazda Tribute, na Ford Escape! Hapo napata kigugumizi niende wapi, kwani mafundi wetu kila mmoja ana sababu zake wengine nissan spear ghali, wengine toyota inakula mafuta sana, ford na mazda, spear hakuna!!! wanajamii naomba msaada na usahuri fasaha!
Umesema unataka SUV, kwnye hiyo orodha yako naona SUV ni Escape na Tribute tu, hizo zingine siyo SUV.
Hzo Mazda na Ford si gari mbaya hata kidogo, tatizo tu ni kwamba ni gari ambazo hazijaenea sana kwenye soko letu, hivyo hata wauzaji wavipuri hawajatoa kipaumbele kuingiza vipuri hivyo, kama hauna pesa ya kwnda kununua origina pale CMC utajikuta unapark gari kwa kitu kidogo sana. Hata mafundi wetu wa bei nafuu uswahilini hawajazijua mifumo yake, unaweza kupleka gari inaugonjwa kidogo tu wanachokonoa na kuharibu zaidi mwisho wa siku wanakwambia KIMEO! Kama uko vizuri, na unausafiri wa ziada pindi unapolazimika kuagiza kipuri nje, au unapoliacha gereji gari lako unalo lingine la kukusogeza basi utazipnda hizo gari ni nzuri.
Tukirudi kwenye mazingira yetu halisi ya kibongo, maisha ya kima cha chini tunalazimika kupleka matngenezo kwa mafundi wa VETA, ni heri hata aliyepitia VETA, wngi hawajapitia huko wamejifunza kwa kutumwa spanner na fundi aliyejifunza kwa kutumwa spanner na fundi ambaye naye hakuwahi kupita chuo, hivyo wanafanya kazi kwa mazowea akikutana na kitu kigeni anakwama, hana vifaa wala njia za kisasa za kujifunza na kukabili kifaa kipya. Lakini hao ndiyo wanaotusaidia kuviweka barabarani vimeo vyetu tunavyookota kwenye jalala la mjapani, hao ndiyo size yetu na wanamsaada mkubwa sana. Hivyo basi tunalazimika tu kununua magari ambayo ni common. Hebu pata picha umenda zako Kiwangwa na family yako, bahati mbaya gari imzingua, kwa gari za kawaida hizi unampigia simu fundi wako anakuja faster anaangalia kama kuna kifaa cha kununua anakimbia gerezani pale anaokota spare anakuja kufunga unarudisha familia nyumbani, ambapo pngine ungelazimika gari kuvutwa na wewe uangalie utaratibu wa kurejesha familia nyumbani kwa njia zingine. Usione magari yote ya mtaani yanafanana Noah, Rav 4, Brevis, Etrail, sjui Mark-X, IST, Vitz, Passo nk. Watu wanalazimika tu kufuata mkumbo ili kujiweka kwenye safe zone!
Sijajua bajeti yako ni ngapi kwenye kununua hiyo gari, lakini kama kweli umeamua kujibana kwnye hayo machaguo basi nunua Noah, tena old model. Kama uko tayari kutoka nje ya hizo, na unataka kubaki kwenye SUV basi angalia RAV 4 old model, X-Trail, kama kabajeti kako vizuri unaweza kwenda hata kwenye Escudo ya kuanzia 2005, Harrier ya kuanzia 2003, au Prado.