Ni gari gani itanifaa kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo?

Ni gari gani itanifaa kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo?

namraroh

Senior Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
114
Reaction score
124
Nataka kununua gari ya kutumia lakini napata taabu kidogo kujua ni gari ya aina gani itanifaa kwa kuzingatia kwamba napenda gari ambayo haizidi cc 2400, iwe na 4 wheel, wenyewe wanita SUV, nimejaribu kuangalia na kuvutiwa na Toyota liteace noah, Nissan Serena, Mazda Tribute, na Ford Escape! Hapo napata kigugumizi niende wapi, kwani mafundi wetu kila mmoja ana sababu zake wengine nissan spear ghali, wengine toyota inakula mafuta sana, ford na mazda, spear hakuna!!! wanajamii naomba msaada na usahuri fasaha!
 
Ni gari yako ya kwanza??!!!
Ukubwa wa familia yako??!
Lengo kusudiwa la gari lako??!!
Wastani wa kipato kwa mwezi????!!
Mazingira itapotumika???!!!!
 
Sio gari ya kwanza, ila napata taabu kwani nakaa Mbezi Luis na kwa miaka ya hivi karibuni inanilazimu kutumia zaidi ya masaa mawili kufika kazini Uwanja wa Taifa Temeke. Familia yangu ya kitanzania watoto wanne!! bado mie na wife!! upo hapo! Matumizi yote kuanzia kwenda kazini, kwenda shamba Kiwangwa, kusafiri kwenda hija Xmas! nakadhalika! kipato nina uwezo wa kuendesha gari mwezi mzima, hapo naona unawezajua kipato changu!
 
Tafuta noah road runner nafikiri itakidhi mahitaji yako. Ni cc 1980 na seating capacity ni 8 pamoja na seat za mwisho ambapo unaweza kuzikunja ukawa na pungufu ya abiria 3 lakini ukaongeza nafasi ya mzigo.
 
Sio gari ya kwanza, ila napata taabu kwani nakaa Mbezi Luis na kwa miaka ya hivi karibuni inanilazimu kutumia zaidi ya masaa mawili kufika kazini Uwanja wa Taifa Temeke. !

Wewe kwa matumizi yako ya kuwahi kazini..........utakuwa unahitaji gari yenye......propeller.......flaps.......landing gear......navigation light........elevator.......flashing beacon na fuselage........na gari yenye vyote hivyo ni Ford Kuga.......wewe tu......kujimwaga.........

CC.... MANI........
 
Last edited by a moderator:

Daah akiagaiza hili na mimi anisaidie kulipata linafaa sana.
 
Last edited by a moderator:
Sio gari ya kwanza, ila napata taabu kwani nakaa Mbezi Luis na kwa miaka ya hivi karibuni inanilazimu kutumia zaidi ya masaa mawili kufika kazini Uwanja wa Taifa Temeke. Familia yangu ya kitanzania watoto wanne!! bado mie na wife!! upo hapo! Matumizi yote kuanzia kwenda kazini, kwenda shamba Kiwangwa, kusafiri kwenda hija Xmas! nakadhalika! kipato nina uwezo wa kuendesha gari mwezi mzima, hapo naona unawezajua kipato changu!

1. Unataka gari kubwa for that matter hayo unayotaja hapo mengi hayakufai. . . .Except hayo ma serena na Noah sijui waaliowahi kutumia, atkeast Noah with 3s ni ngumu yaweza kuwa angukio.
2. Kwa matumizi hayo unayotaja unaendea kwenye SUV's sasa. . . .ambayo kwa shamba itakufikisha ila sio kwa matumizi ya shamba kama ni active project u will need a pick up later on au reverse cycle kama shamba inalipa ongea na wife muweke nguvu huko meanwhile una pick up then faida utawapiga na SUV nao wakubali mzee wao anawawaza na kuwajali.
3. Diversity ya shughuli zako huwezi kuwa na gari moja kwa matumizi yote
 
Nunua mazda hiyo wenzako wanunua bugatti hawaogopi sembuse hiyo ili mradi uwe nahela tu
 
Nataka kununua gari ya kutumia lakini napata taabu kidogo kujua ni gari ya aina gani itanifaa kwa kuzingatia kwamba napenda gari ambayo haizidi cc 2400, iwe na 4 wheel, wenyewe wanita SUV, nimejaribu kuangalia na kuvutiwa na Toyota liteace noah, Nissan Serena, Mazda Tribute, na Ford Escape! Hapo napata kigugumizi niende wapi, kwani mafundi wetu kila mmoja ana sababu zake wengine nissan spear ghali, wengine toyota inakula mafuta sana, ford na mazda, spear hakuna!!! wanajamii naomba msaada na usahuri fasaha!

Umesema unataka SUV, kwnye hiyo orodha yako naona SUV ni Escape na Tribute tu, hizo zingine siyo SUV.
Hzo Mazda na Ford si gari mbaya hata kidogo, tatizo tu ni kwamba ni gari ambazo hazijaenea sana kwenye soko letu, hivyo hata wauzaji wavipuri hawajatoa kipaumbele kuingiza vipuri hivyo, kama hauna pesa ya kwnda kununua origina pale CMC utajikuta unapark gari kwa kitu kidogo sana. Hata mafundi wetu wa bei nafuu uswahilini hawajazijua mifumo yake, unaweza kupleka gari inaugonjwa kidogo tu wanachokonoa na kuharibu zaidi mwisho wa siku wanakwambia KIMEO! Kama uko vizuri, na unausafiri wa ziada pindi unapolazimika kuagiza kipuri nje, au unapoliacha gereji gari lako unalo lingine la kukusogeza basi utazipnda hizo gari ni nzuri.

Tukirudi kwenye mazingira yetu halisi ya kibongo, maisha ya kima cha chini tunalazimika kupleka matngenezo kwa mafundi wa VETA, ni heri hata aliyepitia VETA, wngi hawajapitia huko wamejifunza kwa kutumwa spanner na fundi aliyejifunza kwa kutumwa spanner na fundi ambaye naye hakuwahi kupita chuo, hivyo wanafanya kazi kwa mazowea akikutana na kitu kigeni anakwama, hana vifaa wala njia za kisasa za kujifunza na kukabili kifaa kipya. Lakini hao ndiyo wanaotusaidia kuviweka barabarani vimeo vyetu tunavyookota kwenye jalala la mjapani, hao ndiyo size yetu na wanamsaada mkubwa sana. Hivyo basi tunalazimika tu kununua magari ambayo ni common. Hebu pata picha umenda zako Kiwangwa na family yako, bahati mbaya gari imzingua, kwa gari za kawaida hizi unampigia simu fundi wako anakuja faster anaangalia kama kuna kifaa cha kununua anakimbia gerezani pale anaokota spare anakuja kufunga unarudisha familia nyumbani, ambapo pngine ungelazimika gari kuvutwa na wewe uangalie utaratibu wa kurejesha familia nyumbani kwa njia zingine. Usione magari yote ya mtaani yanafanana Noah, Rav 4, Brevis, Etrail, sjui Mark-X, IST, Vitz, Passo nk. Watu wanalazimika tu kufuata mkumbo ili kujiweka kwenye safe zone!

Sijajua bajeti yako ni ngapi kwenye kununua hiyo gari, lakini kama kweli umeamua kujibana kwnye hayo machaguo basi nunua Noah, tena old model. Kama uko tayari kutoka nje ya hizo, na unataka kubaki kwenye SUV basi angalia RAV 4 old model, X-Trail, kama kabajeti kako vizuri unaweza kwenda hata kwenye Escudo ya kuanzia 2005, Harrier ya kuanzia 2003, au Prado.
 
Hahahaa, kumbe thread ya mwaka jana....lol!

Mkuu naomba ushauri juu ya X trail na Pajero mini aka GDI
nipe uzuri na ubaya wake...

kuna MTU kanikatisha tamaa Sana kuhusu Xtrail
 
Back
Top Bottom