Ni Haki kugomea mashine za EFD

Dumelang

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Posts
3,204
Reaction score
5,710
Kodi ni jambo la msingi, na sioni tatizo la mashine za risiti za EFD
Ila naona haki kubwa walionayo wafanya biashara kugomea hizi mashine.

Juzi tu hapa tulisikia wote mshahara wa Rais mkubwa kiasi kile lakn haukatwi kodi, Yan kiongozi aoneshi uongozi katika jambo la pekee kama hili.

Tuliskia vilevile kwa waziri mkuu mishahara minono lkn isiyotambuliwa na EFD

Hii ni baadhi ya mifano, wapo wengi wakubwa serikarilin na makampun na taasisi zao hawalipi kodi stahiki, wanahisi wafanya biashara hawajui haya, bila shaka wanajua
NDIO MAANA WANAGOMA
hawaoni haja ya kulipa kodi wao wakati wakubwa hawalipi kodi

Makampuni ya simu yanakadiliwa kodi, hakuna mashine inayohakiki mapato yao.

Yapo mengi yakueleza ila lazma tujue mfumo wa utozaji kodi lazima uwe wenye usawa na haki, SI KWA KINDI FLANI TU, BALI NI MUDA TUAMBIWE HATA RAIS PAMOJA NA MAILION YOTE ANAYOPOKEA ANAKATWA KODI.

NA MAENEO YOTE MAKUU, KODI INALIPWA KWA UTHABITI HAPA MIGOMO KAMA HII YA WAFANYA BIASHARA ITAKWISHA, VINGINEVYO. Kazeni uzi nchi haina mwenyewe hii

Mtazamo wangu.
 
naunga mkono hoja.
Utashangaa muwekezaji mwenye mtaji wa mabilioni anapewa msamaha wa kodi tena kwa mika hata mitano lakini mjasiriamali anaebangaiza anabanwa na kuwekewa gharama kubwa.
KODI INATAKIWA ITOZWE KWA HAKI NA KWA WATU WOTE WANAO STAHILI NA SIO KUBAGUA.
TRA WANAACHA KUTOZA KODI KWA WENYE MABILIONI WANA HANGAIKA KUMBANA MTANZANIA WA KAWAIDA ANAETAFUTA RIZKI.
 

Aliyetakiwa kuwa wa kwanza kugoma ni MFANYAKAZI WA KIMA CHA CHINI!
 
Akili ndogo kuongoza akili kubwa. Serikalini hakuna wanafikiri kwa bongo zao bali kwa matumbo yao
 
mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,TRA wana agenda za siri na hizo mashine.Kwa nini wasifanye utafiti wa kina kuhusu hizo mashine na kujua sababu za msingi za wafanyabiashara kugomea.
 
Nawashangaa wenye siraha kuzitumia kuua ndugu zao,badala wazitunze kwani ipo cku kinaweza kunuka hapa nchini! Maana watz wamechoka na manyanyaso! `Tunataka wakubwa nao wakatwe,sio kila siku tunakatwa sisi wadogo tu'
 
mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,TRA wana agenda za siri na hizo mashine.Kwa nini wasifanye utafiti wa kina kuhusu hizo mashine na kujua sababu za msingi za wafanyabiashara kugomea.

Utafiti wa nini wakati tatizo linajulikana. Hujawai kununua kitu kariakoo alafu ukapewa bei ya kitu kama unachukua risiti na bei yachini kama huchukui risiti.

Bongo ukusajaji wa kodi upo chini sana ndio maana wanaleta machine. Hata kenya nao wameanzisha kutumia mashine na watu wakalalamika hivyo hivyo.

Swali la maana ni kwanini watu hawalipishwi kodi sawasawa au kwanini zinaizwa gali. ila kutumia mashine ni kitu kizuri kwasababu inaongeza ufanisi na kupunguza wizi
 
mkuu ni vyema sasa pia ni muda muafaka kwa wasanii wa bongo movie na bongo flava nao kuanza kulipa kodi kila mara wanapofanya kazi zao ziwe jukwaani au hata nje ya jukwaa.hii itasaidia kukuza kipato cha nchi na kuondokana na kuwa omba omba kila mara.
 
hao wakamatwe wafutiwe leseni tu. mimi kama mfanyakazi wa serikali nakatwa karibia laki na nusu kila mwezi kwenye mshahara wangu kama kodi, halafu mfanyabiashara wa kariakoo hataki kulipa kodi? uliwasikia wale wengine wanasema hawataki kutumia mashine, sio kwamba tu wanataka kupunguziwa bei, hawazitaki mashine.
 
Aliyetakiwa kuwa wa kwanza kugoma ni MFANYAKAZI WA KIMA CHA CHINI!

We usipofukuza nzi kwenye kidonda chako na.wezio wakiumia wasifukuze!!!!!????

Hebu amka muda wa kudeki huu utalowana
 

Process ikiwa reasonable and fair hata ukitumia mabavu ku implement wananchi tuta support ila hii ina mapungufu mengi sana ndio maana watu wanachachamaa!!!!!

Kuna mtu analalamikia kukatwa sehemu ya mshahara ili ije imfae uzeeni???!!!!!

TRA wafanye yale yanayitarajiwa bila kuleta kelele zisizo na manufaa
 

Mashine si tatizo, maana kodi ni muhimu, ila suala linakuja hapa huwez kumuhimiza mtoto asivute Bangi wakati baba anakula bangi, serikali ina watu hawalipi kodi, wafanya biashara hawa wanafahamu, wanafahamu pia kulivo huko bandalini na kodi za vifaa vya watu wanaoitwa wazito

Hari itatoka wapi? Kusikia kutatoka wapi wakat najua baba pia mvuta bangi.

Serikali ikaze uzi juu kwanza, wafanyakaz kodi zao hukatwa kwa uaminifu, iwe pia kwa watu ka rais, na wengineo, la sivyo...
MGOMO NI HAKI YAO, INGAWA KODI NI HAKI YA TAIFA
 
hapa siongeleo mafao mzee, kwenye mshahara mfanyakazi unakatwa asilimia 10 inapelekwa huko kwenye mafao, nyingine unakatwa mshahara kubwa kuliko hata hiyo asilimia 10, hivyo kila mwezi mshahara wako unakatwa si chini ya asilimia 20%. unaelewa lakini? au wewe kama mfanyakazi unakatweje mwezetu, hukatwi kodi kumbe?
 

jamaa yako hapo anafikiri ile kodi unayokatwa kwenye mshahara utakuja kuipokea ukistaafu....hajajua kama ndio inayoenda kutumika kuendesha nchi. wananchi wengi kumbe hawana uelewa wa ulipaji kodi hapa tz.
 
We usipofukuza nzi kwenye kidonda chako na.wezio wakiumia wasifukuze!!!!!????

Hebu amka muda wa kudeki huu utalowana

Hahahaha, haya goma!..maana naona wengine wanagoma kwa kisingizio cha bei za mashine, wewe naona unagoma kwa sababu Kikwete halipi kodi, mbaya zaidi unagome JF!!!..Chukua bango uingie mtaani.
 
kuna haja ya kufanya mgomo nchi nzima kugomea wawekezeji walipe kodi au miaka ipunguzwe ili linazewezekana kama tukiamua
 
mkuu ni vyema sasa pia ni muda muafaka kwa wasanii wa bongo movie na bongo flava nao kuanza kulipa kodi kila mara wanapofanya kazi zao ziwe jukwaani au hata nje ya jukwaa.hii itasaidia kukuza kipato cha nchi na kuondokana na kuwa omba omba kila mara.


kama mlishindwa kukaba kodi kwenye madini na sasa yapo mashimo tu
Hata hao wasanii wangetoa akipanga jukwaan pato lake la kwanza chukueni,/
au bongo muv nao ingekuwa muvi yao kwanza hela yake kwa TRA kuombaomba hakutaisha wala umasikini hautaisha coz
viongoz wa nchi hii hawafikirii kutumia ubongo bali wanatumia utumbo!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…