GE2025 Ni haki msimamizi wa uchaguzi ahesabie kura mbali na kituo cha kupigia kura?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Ni moja ya Kanuni ya ajabu eti Msimami wa kituo cha kupigia kura ana uhuru wa kuchagua wapi ahesabie kura. Anaweza kura zikapigiwa say Kimara, akaamua kuhesabia Kigamboni ofisi ya CCM.
Hapa bila Katiba mpya na kuwa tume huru ya uchaguzi hakuna kitu!
Kura yangu ina thamani sana sana!
 
Kaka mayala nakuelewa sana na huwa nasoma sana machapisho yako,juzi kwenye jukwaa la wahariri wa vyombo vya habari ulishauri jambo zuri kuhusu simba wa kizimkazi kushiriki uchaguzi ili chama tawala kisishindane na kivuli chake ili sikumbuki kama kama ushauri wako ulijibiwa,pamoja na juhudi zako za kututia moyo na kuendelea kutuelemisha haya mambo yanakqtisha tamaa!!

Just imagine michezo michafu inayofanyika wakati wa uchaguzi hivi katika hali ya kawaida unapata wapi moral ya kwenda kupanga foleni kupiga kura?

Binafsi hata reforms zikifanyika sipotezi tena muda wangu kwenda kupanga foleni kupiga kura!!
 
Kanuni ya 63:
Mara baada ya kumaliza upigaji kura, msimamizi wa kituo (Presiding Officer) ataanza kuhesabu kura zilizopigwa kwa kila mgombea mbele ya mawakala na waangalizi.
 
Ni ujinga mtupu! Halafu eti yalikaa mijitu mizima yenye watoto wanaowaita baba pole umetoka kazini! Na yanalipwa mishahara na serikali,kupitisha uchafu kama huu!This is rubbish!
 
Uhuni tu, kwa kanuni hii achana na zingine za hovyo, mtu anaweza kuesabia kura akiwa hawara yake , sijui aya yanafanyika kwa faida ya nani, watz tumetelekeza nchi kwa mambo ya hovyo, leo mil 5 au moja inamfanya mtu kutelekeza taifa , Mungu atusaidie watz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…