Augustoons
JF-Expert Member
- Oct 31, 2007
- 409
- 31
Hivi Jamani Nisaidieni,Kwamba ndio njia ya kulazimisha Kujipatia Pesa au ndio staili gani? Wabunge Wetu,Mnasemaje kwenye hili mbona mko kimya? Ni Hivi sasa hivi kumezuka utaratibu mtu ukienda TRA kurenew Road Licence aka Motor Vehicle, kwanza inachukua hadi siku tatu ili uipate tofauti na awali ilikuwa ikipatikana siku hiyohiyo. Pili, unatakiwa ulipie na stika ya Fire sh.40,000, sasa swali langu maana ya kulipia stika ni nini,wakati stikla yenyewe hupewi na pia mtungi wenyewe hupewi? Eti ukiwa nayo hiyo ndio gari lako limekaguliwa kuwa linazingatia sheria ya Zimamoto. Hivi kweli hii kitu Halali?