Ni haki tra kuwalazimisha watu wanapolipia road licence kulipia na sticker ya fire?

Ni haki tra kuwalazimisha watu wanapolipia road licence kulipia na sticker ya fire?

Augustoons

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2007
Posts
409
Reaction score
31
Hivi Jamani Nisaidieni,Kwamba ndio njia ya kulazimisha Kujipatia Pesa au ndio staili gani? Wabunge Wetu,Mnasemaje kwenye hili mbona mko kimya? Ni Hivi sasa hivi kumezuka utaratibu mtu ukienda TRA kurenew Road Licence aka Motor Vehicle, kwanza inachukua hadi siku tatu ili uipate tofauti na awali ilikuwa ikipatikana siku hiyohiyo. Pili, unatakiwa ulipie na stika ya Fire sh.40,000, sasa swali langu maana ya kulipia stika ni nini,wakati stikla yenyewe hupewi na pia mtungi wenyewe hupewi? Eti ukiwa nayo hiyo ndio gari lako limekaguliwa kuwa linazingatia sheria ya Zimamoto. Hivi kweli hii kitu Halali?
 
Nchi hii kila kiongozi wa taasisi hata kama ni ya kuongoza mtaa
eti naye ana mamlaka kamili ya kujifanyia anachotaka, hata
kujitungia sheria zake...
 
Sicker ya Fire ni kuthibitisha kwamba fire extinguisher yako imekaguliwa na umelipa gharama ya ukaguzi. TRA wameshaanzisha kitengo cha kukagua fire extinguisher. Wabunge wetu mpaka kitu kiwe kinawaathiri wao binafsi ndio wanakisemea subiri kwa vile wataathirika na usumbufu huu tutawasikia wakilisemea.(wana mabasi, malori, daladala) Poa tu hii kero itaondolewa.
 
Hapana ile inaitwa fire inspection fee..unatakiwa ndani ya siku 7 uende fire ukakaguliwe hapo ndipo utapewa fire sticker for free(kwa kuwa utakuwa umelipia)sio kila chombo cha moto kinatozwa elfu arobaini...hapana inategemea na ukubwa wa engine(cc)kumbuka ukienda fire nenda na mtungi wako ili waukague...hakuna kitengo kimeanzishwa na TRA kuhusu fire masuala yote yahusuyo moto bado yapo chini ya kikosi cha zimamoto TRA unalipa inspection fee tu na si vinginevyo...taratibu hii imeanza tarehe 23.07.2012
 
Back
Top Bottom