Tupe tofauti
Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
Wajibu ni kitu ambacho ni lazima ukifanye.
Kwa mfano, mfagizi wa ofisi ana wajibu wa kufagia ofisi ili kupata ujira wake.
Haki ni kitu ambacho unaweza kukipata ukikitaka lakini si lazima ukipate.
Kwa mfano.
Watanzania wenye miakazaidi ya 18na wasio wafungwa wana haki ya kupiga kura kumchagua rais.
Ukiuliza kamawazaziwana hakiya kumsaidia mtoto kupata mtaji, wanayo haki hiyo. Wakimsaidia hakuna atakayewashitakikwa sababu hiyo au kuwasema vibaya, kama mtu ambaye akipiga kura kwa stahili yake ya uraia hakuna atakayemshitaki wala kumsema vibaya.
Swali ninaloliona hapa ni la wajibu.
Wazazi wana wajibu?
Wajibu unaendana na ulazima.
Je, ni lazima wazazi wampe mtaji mtoto? Wazazi wasipompa mtaji mtoto, itakuwa sawa?
Kwangu mimi, wazazi wote wana wajibu (wanalazimika) wa kumuelimisha mtoto. Huo ndio mtaji muhimu kabisa wa kuanzia maisha. Zaidi ya hapo, kumzidishia mambo ya mtaji wa biashara ni haki yao (wanaweza kufanya hilo) lakini si wajibu (hawalazimiki kufanya hilo).