Ni haki ya mzazi kukupa mtaji wa kuanzia maisha /biashara?

Ni haki ya mzazi kukupa mtaji wa kuanzia maisha /biashara?

THNKER-hardson

Senior Member
Joined
Dec 26, 2016
Posts
150
Reaction score
80
Vijana weng husubiri mtaji au urithi kutoka kwa wazazi
Je kuna ulazima upate uo msaada ili kuanza maisha au..?
Maana wazee wa zaman wengi waliwapa watoto wao shamba au elimu kama urithi

Mzazi ajanipa urith wa vyote naweza subiri mali zake[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Tupe tofauti

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app

Wajibu ni kitu ambacho ni lazima ukifanye.

Kwa mfano, mfagizi wa ofisi ana wajibu wa kufagia ofisi ili kupata ujira wake.

Haki ni kitu ambacho unaweza kukipata ukikitaka lakini si lazima ukipate.

Kwa mfano.

Watanzania wenye miakazaidi ya 18na wasio wafungwa wana haki ya kupiga kura kumchagua rais.

Ukiuliza kamawazaziwana hakiya kumsaidia mtoto kupata mtaji, wanayo haki hiyo. Wakimsaidia hakuna atakayewashitakikwa sababu hiyo au kuwasema vibaya, kama mtu ambaye akipiga kura kwa stahili yake ya uraia hakuna atakayemshitaki wala kumsema vibaya.

Swali ninaloliona hapa ni la wajibu.

Wazazi wana wajibu?

Wajibu unaendana na ulazima.

Je, ni lazima wazazi wampe mtaji mtoto? Wazazi wasipompa mtaji mtoto, itakuwa sawa?

Kwangu mimi, wazazi wote wana wajibu (wanalazimika) wa kumuelimisha mtoto. Huo ndio mtaji muhimu kabisa wa kuanzia maisha. Zaidi ya hapo, kumzidishia mambo ya mtaji wa biashara ni haki yao (wanaweza kufanya hilo) lakini si wajibu (hawalazimiki kufanya hilo).
 
Ni haki kupata chochote kutoka kwa Wazazi ila ni Wajibu wangu kuwapa urithi watoto wangu.......!
 
Back
Top Bottom