Ni halali kujengea makaburi?

Ni halali kujengea makaburi?

Mimi binafsi sioni tatizo katika hilo, nimejengea kaburi la Baba, mama na mdogo angu.

Na kila wakati nafika pale kuzungumza nao maana naamini nafsi zao zinaishi pamoja nami.

Tatizo kubwa Waafrika tulipoteza asili yetu na kukumbatia asili ya wazungu/ waarabu kwa mwamvuli wa Dini.
Umemaliza kila kitu mkuu.Umewahi kusoma "Theology of African Traditional Religion"?.Aisee kuna Elimu nzuri sana humu.
 
Hili swali nalileta kwa waumini wa pande zote Waisilamu na wakristo,ili tulijadili kwa pamoja ni halali au hairusiwi kujengea makaburi?
Kuandika majina ya marehemu,tarehe walizozariwa na tarehe za siku waliyokufa?
Makaburi yanajengwa kwa ajili ya kumbukumbu kwa ndugu zake na familia yake,kuandika majina tar ya kuzaliwa na kufa ni sehemu ya iyo kumbukumbu..Anaefanya anafanya na asieona umuhimu anaweza asifanye pia, Uhalali wa kujenga kaburi Ama kutokujenga ni utashi wa jamii husika,huwezi kupata majibu ya Yenye usawa kwani Wakristo na waislamu kuna sehemu tunapishana

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
 
Binadamu aliumbwa kwa udongo na atarudi kuwa udongo,maana yake mtu anapokufa, anazikwa.Mwili wake na mifupa yake yote hubadilika kuwa udongo ndiyo tafsiri yake

Maana yake haina haja ya kumzika na nguo au jeneza na mavitu ya ghalama, maana siku ya kufufuliwa kila mtu atafufuliwa uchi wa mnyama

Ukija upande wa kaburi, hairuhusiwi kujengewa wala kuandika majina ya marehemu, maan uzuri wa marehemu au ubaya wake unatokana na yale matendo aliyoyafanya akiwa hai duniani, siyo kujenga na kuremba kaburi tukitarajia labda tunamuhesimisha marehemu.

Na kama marehemu aliiacha kizazi chema mfano watoto waliosoma dini au Quruani basi watatumie elimu yao kumuombe mzazi wao,
Unadhani kwann makaburi ya zamani yalichongwa,kama lile la Yesu ambalo watu walikua wanaenda kumsabahi waliempenda ? Makaburi kujengewa ni muhimu yasipotee
 
Makaburi yanajengwa kwa ajili ya kumbukumbu kwa ndugu zake na familia yake,kuandika majina tar ya kuzaliwa na kufa ni sehemu ya iyo kumbukumbu..Anaefanya anafanya na asieona umuhimu anaweza asifanye pia, Uhalali wa kujenga kaburi Ama kutokujenga ni utashi wa jamii husika,huwezi kupata majibu ya Yenye usawa kwani Wakristo na waislamu kuna sehemu tunapishana

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
Mathayo 23:27 enyi wanafiki mnayapaka makaburi chokaa, na kuyapamba kwa mapambo mengi.lakini ndani yake yamejaa mifupa na uchafu.(unafiki)
 
Haitakiwi kuacha alama ya mtu akifa,maana kusema tu lile kaburi la fulani ni shiriki

kabla ya miaka 5 ya kufa mtume Muhamad (S.A.W)alikataza kabisa kuhusu kujengea makaburi ili watu wasije wakayaabudu na kugeuza sehemu za kutatulia shida zao

Lakini siyo kwamba mtu anakatazwa kwenda kuyatembelea makaburi,anaruhusiwa ila ambacho hakitakiwi ni kule kusema lile la shangazi lile la baba lile la fulani,hii ndiyo imekatazwa
Unaweka na rejea sasa sio unaandikaandika tu ,tutaaminije.weka rejea tuone palivyoandikwa hivyo
 
Yaani kusema tu lile la fulani ni dhambi,sababu yule mtu ategeuka na kuwa mafuvumbi,sasa kuna uhalali gani hapo wa kujua aliyelala ni furani,lakini ni haki kuwasalimia kwa ujumla watu wòte wa makaburini,mu hali gani sisi wote huku ni wazima na si mda mrefu tutaungana nanyi pamoja makuburini
Umeandika utumbo kama unabisha soma tena ulichoandika
 
عن أبي الهياج الأسدي قال: قال لي علي رضي الله عنه : «ألا أَبْعَثُك على ما بَعَثَني عليه رسول الله صلى الله عليه وسلم ؟ أن لا تَدْعَ صُورَةً إلا طَمَسْتَها، ولا قَبْرًا مُشْرِفًا إلا سَوَّيْتَه». صحيح] - [رواه مسلم

Kutoka kwa Abii Hayyaji Al-Asadiy Amesema: Alisema kuniambia mimi Ally -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: "Je nikuagize katika yale aliyoniagiza kwayo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake? Usiache picha yoyote ispokuwa umeifuta, wala kaburi lililonyanyuliwa ispokuwa umelisawazisha".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

نْ جَابِرٍ (رضي الله عنه) قَالَ: نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يُجَصَّصَ الْقَبْرُ وَأَنْ يُقْعَدَ عَلَيْهِ وَأَنْ يُبْنَى عَلَيْهِ. مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kaburi kutiwa chokaa (liwe imara), kuketiwa juu yake na kujengewa. [Muslim]
Yaani abi hayyaj na jabir wawe muongozo!?..hata kuwafahamu unawafahamu,una uhakika walikuwepo!?..Kuna alikiri kutunga Hadith 2500 na zikapitishwa kuwa sahihi,alipopelekwa kwa khalifa kwa mashtaka hayo,kesi haikufika mwisho akauawa na wahafidhina,hakutanabahisha alitunga zipi?..ummar (ra)alipiga marufuku Hadith,alizuwia wahyi!?
 
Binadamu aliumbwa kwa udongo na atarudi kuwa udongo,maana yake mtu anapokufa, anazikwa.Mwili wake na mifupa yake yote hubadilika kuwa udongo ndiyo tafsiri yake

Maana yake haina haja ya kumzika na nguo au jeneza na mavitu ya ghalama, maana siku ya kufufuliwa kila mtu atafufuliwa uchi wa mnyama

Ukija upande wa kaburi, hairuhusiwi kujengewa wala kuandika majina ya marehemu, maan uzuri wa marehemu au ubaya wake unatokana na yale matendo aliyoyafanya akiwa hai duniani, siyo kujenga na kuremba kaburi tukitarajia labda tunamuhesimisha marehemu.

Na kama marehemu aliiacha kizazi chema mfano watoto waliosoma dini au Quruani basi watatumie elimu yao kumuombe mzazi wao,
Kila kitu kilicho juu ya ardhi mwishowe kinakuwa udongo mkuu. Uwe umezikwa na jeneza au sanda au kabur kujengewe ni yale yale tu so kila mtu azikwe vyovyote mwishowe ni udongo. Tatizo hapo ni muda tu northing more
 
Back
Top Bottom