Ni halali kumuacha mkeo kisa hajui kupika?

msichana mvivu wa kitandani utamjua tu, vitu vidogo dogo kama hivyo anakuwa anashindwa ati!
katika wale wote niliobahatika kuwa nao, mashalllah wamebarikiwa vyote viwili!!
hamna ukweli wowote,kutokupika si uvivu ila pia si kigezo cha uwezo wako kitandani atii,ila wanaume mnakuza mambo sana
 
Si anakushangaa hutaki kupika ugali....!!!!!!!
mhh ugali sipiki kweli kabisa,cha kukomaza mikono yangu,inatakiwa iwe lainiiiii ili kuikamata mic tu na sio miko ya ugali,ugali wenyewe wa kisukuma mgumu huo unapika mpaka mikono inatoka sugu inahusu!!!
 
kama alikuwa anampenda kweli asingemfukuza bali angekaa naye na kumuuliza vizuri tatizo ni nini, na baada ya hapo basi alitakiwa amfundishe kupika. Huo ni ubavu wako yaani kupikiwa tu unarudisha mke tena wa ndoa kabisa..mmh
 
Huyu hakuwa anatafuta mke bali mpishi wa kumpikia.
 

Hao ndo wanasema nimepata jiko. Kwa nini mkeo umsongeshe ugali wakati vyakula kama ndizi vipo? Kusonga ugali ni suluba na unamkomaza mkeo. Kusonga ugali ni mazoezi ya viungo, sio upishi.
 
Ndo tatizo la Wanaume wanaojua kupika sana!!
Pls jamani Wababa 2ache kujipikilisha ili tusiwakosoe sana hawa wamama!!!
Sijasema tusijue kupika ila tupunguze maujuzi sana!!!
 
Huyu hakuwa anatafuta mke bali mpishi wa kumpikia.

Jamaa alikuwa anatafuta mke. Lakini katika utamaduni wa Kiafrika,kitanzania wa kimila, mke ni "total package"; kushughulikia nyumba, kumliwaza bwana/mume, kulea watoto, kudhibiti "jiko" na kazi za ofisi hiyo na shughuli za shambani.

Leo , ndiyo kuna hizi haki ya mwanamke, imekuwa fujo tupu, hajulikani nani mume nani mke... wanawake wasomi na wakazi wa mijini ndio wamepata nini tena kila kitu wanasema ni unyanyasaji wa jinsia...majumbani hamkani..amani haipo tena.. wacha waume wajitafutie vimada na kinamama wanalalamika..dunia imekuwa uwanja wa fujo,ushindani wa kijinsia, ndio maana ulesbian umeingia kwa nguvu sasa,zamani ulikuwepo ule mchezo mbovu wa midume tu..sasa loooh.. ushindani japo kwa kutumia uume wa plastiki.. mambo mbele kwa mbele...... mpaka tutie akili.
 
sasa alioa wa nini huku ukijua hajui kupika? au ndio chagulaga?
 
usilegee bwana utanlegeza na mie,ila ugali sipiki tuambiane mapema

Tutaelewana tu ukishaingia ndani,si umependa msukuma mama....
mhh vinginevyo nao pia ungewachakachua

Na wala hkuna ambaye angeshangaa...
mhh ugali sipiki kweli kabisa,cha kukomaza mikono yangu,inatakiwa iwe lainiiiii ili kuikamata mic tu na sio miko ya ugali,ugali wenyewe wa kisukuma mgumu huo unapika mpaka mikono inatoka sugu inahusu!!!

Ungejua jinsi mike zetu tulivyozikomaza siku hizi, ungepika tu huo ugali angalau ukiishika nami nihisi nimeguswa...
 
Tatizo letu tunapenda ready made. Kwani kupia ni sayansi, ni kitu ambacho ni relative. Wengie ubwabwa wabauwezea, wengine sembe ndoo umefika, etc.

Halafu mapishi yetu ya kin=bongo ukimpa mzungu ataona ni matope. Maana yeye amezoea kula vimajani vyake ambayo hatahavijachemshwa.

Kwa hiyo kama kweli kapika ugali mbichi inategemea maana kule kwetu ugali ukisha iva wanatia maji tena. Sasa usije kuoa kwetu ukamfukuza, TUTAKUTIMUA HATA KABLA HUJAPEWA MWALI.

Pia ADAMU alipo pewa eva, sio kwamba eva alikuwa mzuri katika kila kitu, alikuwa mshamba katika mambo mengi, lakini walifundishana hadi mambo yakanyoka.

Iweni na shukrani , watu wanachnganyikiwa kwa kukosa wenza wa maisha halafu nyie mnawafukuza??
 




Kha jamani yaani umbali wa km 20 tu asijue kupika ugali?Hata kama nimemtoa sehemu ambayo hawali ugali iweje ashindwe kula ugali,hivi kuna watu ambao hawali ugali siku hizi?Mbona mpaka wamasai wanakula ugali?
 
Mambo yakizamani siyo zama hizi!!kwani yawezekana demu hajawahi kupika kwao kulikuwa na watumishi kibao kiasi kupika hakushughulika!!hivyo kwanini amrudishe nindoa za ngumbaru.
 
Mambo yakizamani siyo zama hizi!!kwani yawezekana demu hajawahi kupika kwao kulikuwa na watumishi kibao kiasi kupika hakushughulika!!hivyo kwanini amrudishe nindoa za ngumbaru.



Mh KK kumbe ndio mnavyowaharibu watoto wenu siku hizi?
 
Usukumani kutokujua kupika especially ugali ni disqualification kwa wakwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…