Ni halali kumuacha mkeo kisa hajui kupika?

mhh ugali sipiki kweli kabisa,cha kukomaza mikono yangu,inatakiwa iwe lainiiiii ili kuikamata mic tu na sio miko ya ugali,ugali wenyewe wa kisukuma mgumu huo unapika mpaka mikono inatoka sugu inahusu!!!

Hata mic za kisukuma sio lelemama, unaimba hasa watu mpaka kushangilia laziam ujue kuimba mama....
 
Bibie kanuna ile issue ya jana, nipo tu nang'aa macho kwa jamii forums...

hahahahah lol
pole sana mtu wangu hamna dozi leo...
mmmhhhh piga magoti yaishe..
maana kwa kweli hutashinda kwenye hili lol...
 
Karibu mkuu jukwaani,sasa hapo tunawanyanyasa vipi,sijaelewa ati,ina maana hata wakishindwa majukumu yao nasi tukachukua hatua inakuwa ni kuwanyanyasa?

tunawafumania lakini hatuwaachi kutokujua kupika tu ndio talaka jamani!
 
tunawafumania lakini hatuwaachi kutokujua kupika tu ndio talaka jamani!
Nakubaliana nawe mizani kidogo inatupendelea wanaume,BTW nashukuru kwa offer yako ya kuniliwaza Cheusi alivyoenda kuhesabiwa nilikuwa bado sijashukuru,asante kwa moyo wa upendo.
 

Hapo kwenye bold, unataka leo niamini tofauti na siku zote kwamba wewe si Mama Mchungaji bali Baba Mchungaji? Maana kama na wewe ni mwanaume anayelalamikia hali hii! Mimi kama mwanaume nakwambia usijali.
 
Usukumani kutokujua kupika especially ugali ni disqualification kwa wakwe

Hakuna kitu kinaitwa 'kupika ugali' ila 'kusonga ugali'. By definition kutoka Buhaya encyclopeadia, kusonga ugali ni mazoezi ya viungo na wala si upishi. Nenda vyuo vyote vya hotel management, hakuna kozi ya kusonga ugali. Kuleni ndizi na wali, msiwatese wake zenu au wafanyakazi wenu wa ndani.
 



Eti tule ndizi,kwani sisi tumbili?Wengine watatuambia tule wali,kwani tumekuwa ndege?Si mimi ni misemo ya wasukuma hiyo.
 
Mimi napika mashed potatoes na pancakes, macaroni, ugali tu ! Ndio mwisho wa ufundi wangu! Dishes zingine tunasaidiana wala sitanii...wala siachiki, kwakuwa hicho hakikuwa kigezo cha kuwekwa ndani,
No matter how hard I try the other stuff..it just embarass so we just have to do it together coz he's better than me, the nice part is...its so much fun and it brings us closer and closer, I love sunday cooking....🙂 🙂
Thts why baby I thank u daily for loving me for who I am and not what I can offer, either in bed or in kind!
Mbarikiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…