Hapa ndio utajuwa mafundisho ya ndoa ya Kiislam kuwa ni mema.
Kwanza, kiIslam hakuna kuowa, kuna kuoana.
Pili, Hakuna kuacha mke kama hajui kupika, kwanza hili kabisa halimo, mwanamke katika mafundisho ya ndoa za kiIslam hatakiwi kupika, kufuwa wala kuhangaika na makazi ya nyumbani ila kwa kupenda na kutaka mwenyewe, ikiwa atafanya hakatazwi.
Mume ndie anaepaswa kulishwa, kuvikwa na kuenziwa. Yeye akae kama pambo la nyumbani, sio unakuja unakuta mkeo mikono ina visuguu kwa kufanya makazi ya nyumbani, hata akikupapasa utafikiri unapitishiwa msasa, Haitakiwi. Mwanamke akikushika inatakiwa mikono iwe laini, usikie raha.
Huyo alieach mkewe kwa kuwa hajui kupika, si angemfundisha? au angekuwa anampikia yeye, kwani lazima mwanamke apike?