wadau Hiki kitu nimekuwa nacho moyoni nadhani huu ni mwaka watatu sasa, Kwa tulio wengi tunajua Malengo ya kuanzishwa kwa SOKOINE UNIVERSTY - MOROGORO ni nchi iwe na wataalamu wakutosha wakilimo, ni wazo jema kabisa, ila kilichonishangaza ni hao wasomi wa chuo hicho kuanzisha televison( SUA TV) nadhani ni Tv ya kwanza kumilikiwa na chuo kikuu hapa Tanzania, moyoni najiuliza ni kwa nini wasingeanzisha kiwanda cha maziwa na nyama?????naamini pesa mlizotumia kuanzishia hiyo TV zingetosha sana tu kwa hilo lengo, mtajitetea na kusema ni pesa za wafadhili na jiuliza mlishindwaje kuwa na hilo wazo kama mlitaka kuonekana SEREKALI si ina TV yake ambayo mgeingia nao mkataba wawe wanaonyesha mambo mliyokuwa mnataka jamii iyaone??? Hamkuona kiwanda cha maziwa hata bna baadae cha nyama kingekuwa na manufaa zaidi kiliko hiyo TV??naamini nyie ndo mlikuwa watu wa kwanza kuwa na mashamba ya mfano na hicho kiwanda ambacho naamini hakingewagarimu pesa nyingi kihivyo kuliko hiyo TV.Mbona wakenya wameweza? Chuo kikuu cha Egerton ni chuo cha kilimo kama nyie wameweza kuanzisha shamba la ngome na wana kiwanda cha maziwa ambacho kinatumika kama sehemu ya wanafunzi kujifunzia na maziwa yao wanayauza miji mbalimbali kya kenya kwa kupitia mawakala.
Wananzuoni wa SUA badilikeni,hata hiyo TV yenu haionekani maeneo yote ya morogoro mgekuwa mnatuzalishia maziwa naamini yangesambaa karibu TZ yote na kutoa fursa kwa wanafunzi kujifunza
Wadau nawakilisha??????
Binafsi ninakushangaa - Prodigal Son - kama kweli wastahili kuwa na jina hilo. Kwa ninavyoelewa mimi, Prodigal Son ni kijana ambaye ana upeo mkubwa wa kuona mbali, jambo ambalo, kama ungetafakari kwa kina ungeelwa SUA wana mtazamo gani kwa kuanzisha hiyo TV. Kwa kuwa sikuwa na taarifa kwamba tayari imeanzishwa, nawapa pongezi kwa kufanya hivyo.
Suala ni, kwa nini SUA wameanzisha TV BADALA YA kiwanda cha maziwa, kama unavyotoa hoja yako.
Ndio, SUA ni chuo kikuu cha kilimo, na iko kwenye mantiki yao kuwa na kiwanda cha maziwa. Je, unafahamu kama kiwanda hicho - hata kama kina uwezo mdogo - kipo au hakipo?
Kuhusu kwa nini SUA wameanzisha kituo cha TV, jibu lake ni rahisi sana. Kama nyote mnavyoelewa, kwanza, wataalam wa ugani (agricultural extension officers) ni wachache sana nchini mwetu, na hata hao wanaosomea fani hiyo, wengi wao hukimbia kwenda mikoani wanapopangiwa, kwa kuwa wanaona kwamba mikoani kuna hali duni ya maisha. Kwa hiyo, wataalam wa SUA wameona kwamba, kituo hicho cha TV kinaweza kutoa mafunzo na/au maelekezo ya ugani, ili kuwafundisha wakulima kilimo cha kisasa, kwa kuwa TV inaweza kuonekana mbali zaidi na kuwafikia watu wengi zaidi, kuliko uwezo mdogo wa maofisa ugani.
Suala la kwamba TV hiyo haionekani kila mahali ni la kisheria zaidi. Kwa mujibu wa sheria ya mawasiliano, inayosimamiwa na TCRA, kila anayeanzisha kituo cha redio na/au TV, anapewa leseni ya muda ya kutangaza kwenye kiwango kinachoitwa District, yaani, ndani ya wilaya yake tu, kwa muda wa mwaka mmoja. Hii inawekwa kwa sababu ya angalizo; je, mtangazaji na uwezo wa kudumu katika soko? Je, vipindi vinavyoandaliwa vina manufaa yoyote yale kwa jamii na havikiuki maadili ya Kitanzania? Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo TCRA wanayapima na kuyafuatilia, kwa muda wa mwaka mmoja, kabla ya kukaa kikao na kutoa leseni mpya inatakayomwezesha mtangazaji kufika nchini kote.
Kaka, kama ulikuwa huelewi ni kwa nini SUA-TV haionekani kila mahali, ungeuliza, kuliko kukurupuka na kuanza kubwabwaja maneno yasiyo na msingi.
Kuuliza si ujinga. Ficha upumbavu wako, usifiche hekima zako.
./Mwana wa Haki
P.S. SUA wanapaswa kuwa na TV PAMOJA NA kiwanda cha maziwa. Lakini wapo wawekezaji ambao wanaweza kuwekeza kwenye kiwanda. SUA ni wataalam wa kilimo, TV itasaidia kuwafundisha Watanzania kuhusu ukulima wa kisasa! Bila elimu, Kilimo Kwanza HAITAFANIKIWA! Tumaini University, nanyi mmejiandaaje kuwapa wananchi mnachofundisha?