Ni Halali Watoto wa Nje ya Ndoa Kuwaita WANAHARAMU???

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Wanajamvi,

Japo huenda ninahitaji kupata fasiri yakinifu ya neno nje ya ndoa na japo waswahili wanasema
kitanda hakizai haramu, ningependa kushirikisha hii kadhia ya watoto wanaoitwa wanaharamu!! wenzangu hii imekaaje??


kuna perspective nyingi kuhusiana na majaliwa/mustakabali wa watoto hawa, kwa mujibu wa sheria za Tanzania, Mtoto wa aina hii anaweza kurithi pale tu aidha atakapokuwa amehalalishwa katika familia husika au mzazi kuacha wosia, kwa kimila inategema na uhalalishaji wa huyo mtoto kwa kufuata mila na desturi husika na kuna baadhi ya dini
ambapo hawana haki kabisa ya kurithi (HARAMU)

lakini tunapoona ongezeko kubwa la watoto katika mitaa (si wa mitaani) n.k naomba utoe maoni yako kuhusu mada hii, haijalishi kama wewe ni mmojawapo au la!! Mimi ni mmojawapo amabye anakerekea sana na unyanyaswaji wa kundi hili.

Nawasilisha
 
haramu zote tamu.
Haramu kwako, halali kwa wenzio.
 
Hakuna mtoto wa mgongoni na wa tumboni wote ni watoto! TutataJaji zaidi!
 
....Mie kwa maoni yangu si halali, kwa sababu wao hawana kosa lolote lile liliosababisha wazaliwe nje ya ndoa na kama wangekuwa na uwezo wa kuamua wazaliwe katika mazingira yepi, basi wasingeafiki kuzaliwa katika mazingira yaliyojaa utatanishi ambao unaweza kuwaletea dosari kubwa katika maisha yao yote hapa duniani.
 
katika taratibu za iman yangu...ilipokatazwa watu wasizini(kutenda tendo la jimai nje ya ndoa) ilikua inaepushwa haki hizi za watoto .
Kama mnaona ni sawa ...maana yake kwenu zinaa ni sawa. Hapo itakua ni tatizo.
Pia mtoto wa nje ya ndoa si haram. Haramu ni watu waliomo nadani ya ndoa wakala vyakula vilivyosababisha urutubisho wa huyo mtoto...ndipo ataitwa mtoto wa haram.

Na hii inaweza kua wazazi wengi japo wamo ndani ya ndoa zao lakin watoto zao ni wana haram. Mungu atunusuru.
 
mbele ya jicho la mzazi watoto wake wote huwa ni halali,ya haram yanaletwa na wale ambao hawakumzaa huyo mtoto na hao,i dare say,they should mind their own business!
 
Kama pia wewe ni msomaji wa Biblia vipi kuhusu Ibrahim na watoto wake wawili i.e Isaka na Ishmaeli ambapo Ishmaeli alikuwa ni mtoto wa Kijakazi (house girl) na Mungu akamwambia Ibrahimu kuwa Ishmaeli hatarithi mali zake isipokuwa atambariki Ishmaeli. Matokeo yake unaona leo Waarabu wamejaliwa utajiri wa mafuta. Je Mungu alikosea kutomtambua Ishmael?
 
kumuita mwanaharamu si sahihi kabisa kwani hakupenda iwe hivyo
 
Na vipi kuhusu Yoseph kumpokea Yesu awe mwanae na hali hakuwa wake?

Ingekuwaje angemkataa?

 
Ni kweli kabisa... Ni ubaguzi mbaya sana

Sio haki kabisa kwa hao watoto,alafu utakuta watu hao hao wanajifanya wameshikilia dini zinazowafunza kutohukumu.
 
Si haki kuwaita watoto haramu kwani hawakupenda kuzaliwa nje ya ndoa. Mimi naona inabidi nao wapewe haki sawa kama tu watoto wengine waliozaliwa ndani ya ndoa.
 
Na vipi kuhusu Yoseph kumpokea Yesu awe mwanae na hali hakuwa wake?

Ingekuwaje angemkataa?

Suala la kuzaliwa kwa Yesu ni tofauti kwa sababu hakuzaliwa kwa mbegu ya kawaida ya binadamu. Pia inasaidia watu kuheshimu ndoa zao halali, kama una mtoto wa nje ni vizuri umtengenezee mazingira yake ya kujitegemea vizuri kabla haujafa (mzazi) ili kutosababisha matatizo katika familia
 
Kajifunze vizur iman...
Ipi iman(deen) yako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…