Hapana mkuu hujanikwaza! Na wala sikulazimishi kukuvutia kwenye imani yangu bila ridhaa yako. Huo ni uwamuzi wako.
(1) Umeuliza:Hivi mtu unakaa chumba kimoja cha kupanga utaacha urithi gani dnia hii? Nami nikaeleza hivi, kurithi ni haki ya mtoto.si lazima uwe umeacha magari,nyumba na vinginevyo chochote utakachokiacha hata kama ni kijiko atakirithi.
(2) Ukasema tena: na kwa nini ifikiriwe kwamba watoto kazi yao ni kurithi tu na sio wao kumiliki mali na wazazi wao ndio waje kurithi kama mtoto ataanza kufariki.
Kwanza nikueleze tu ya kuwa kurithi sio kazi. Kurithi ni haki ya mtu. Hata kama warithi walishajitafutia mali zao,lakini bado wao wana haki ya kurithi mali zilizoachwa na wazazi wao,au wazazi kwa watoto wao au ndugu wengine pia. Na urithi unakuja baada ya mrithiwa kuaga dunia. Si kweli kuwa mrithi hawezi akajishughulisha katika kujitafutia mali yake au mzazi akamuwekea misingi mtoto wake eti 7bu tu atakuja kurithi mali za wazazi wake hapana!
(3) Hizi dini msizifuate kama misukule, changanyeni na akili zenu.
Ufahamu tu kuwa dini ni mfumo wa maisha ambao binadamu anatakiwa awenao katika kila siku ya maisha yake hadi mwisho wa uhai wake. Sasa kwa vile wewe ni mpagani,huwezi kulielewa somo hili kutokana na kile unachoamini!