Ni Halali Watoto wa Nje ya Ndoa Kuwaita WANAHARAMU???

si haki kumwita mtoto fulani 'mwanaharamu'
 
Naomba nichangie kidogo kuhusu neno haram.
Neno hili ni la kiarabu likiwa na maana ya 'katazo kubwa'(forbidden) ambalo mwenyezi mungu amelikataza. Kwamba ukifanya tendo hilo utakuwa umetenda dhambi.

Kati ya matendo hayo ni; uzinifu, mauaji au ushoga.
Pia lipo kundi la vyakula kama Nguruwe na vinywaji kama pombe.

Maana haiishi hapo, hata kitendo cha kula mchana wakati wa mfungo bila sababu iliyoanishwa kidini ni haram. Hapa tunaona kuwa chakula si haram bali tendo ndio haram kama ambavyo mtoto si haram bali tendo lililofanyika.
Kwa msingi huo haram sio kitu bali ni tendo linalopelekea mtu kuingia katika dhambi kwa mujibu wa kiarabu.

Sisi waswahili tumelichukulia kama jina na kitu. Mtoto wa haram haina maana anaitwa haram, ina maana mtoto aliyepatikana kwa tendo lililokatazwa na linalopelekea mtu kupata dhambi ambalo ni 'adultery' kama ilivyoelezwa hapo juu.

Kwasababu za tafsiri za lugha zisizo sahihi mtu anakatisha kwa kusema mwanaharam kama jina la mtoto yule. Ni makosa!! pengine alitakiwa basi aseme mwana wa haram akimaanisha mtoto aliyepatikana katika mazingira ya dhambi ingawaje bado haina ladha .
Hii haina maana yeye ni dhambi, hapana! ni kuonyesha upatikanaji wake ulikuwa vipi. Kama ni sahihi au la hapo wasomaji watapima, nilichokusudia ni kutoa maana kwa upana wake.

Kule milimani Upareni wanatumia neno 'nzune' kama dhambi. Tofauti na wengine wao husema 'mwana wa nzune' wakimaanisha mtoto nje ya ndoa ikiwa inabidi na husemwa kwa stara isiyo na maudhi,lakini ni mwiko mkubwa na ni tusi kumwita mtoto huyo nzune. Hapo ndipo ilipo tofauti na waswahili wanapomwita mwanaharam kama jina.

Ni mchango kidogo kadri ninavyoelewa na inaweza kuwa wapo wenye maana zaidi au tofauti.
 
Kama ni uharamu watakuwa nao wazazi wao waliowazalia humo nje ya ndoa
 
Kama ni uharamu watakuwa nao wazazi wao waliowazalia humo nje ya ndoa
Na wala wazazi sio haram, haram ni lile tendo nje ya taratibu za jamii husika inayokubaliana na definition hiyo.
 
Kajifunze vizur iman...
Ipi iman(deen) yako?

Soma Biblia kitabu cha Mwanzo Sura ya 21 yote halafu ndiyo uniambie au unielekeze nilipokosea. Cha muhimu ni "citation" siyo dini yangu. Na siyo "haki" zote zinazopigiwa kelele na binadamu lazima zifanane na "haki" za Mungu. Ni sawasawa na kupigania haki za mashoga(jinsia moja) ambapo kibinadamu (kwa baadhi ya watu na mataifa) inaonekana ni sahihi ingawa kwa Mungu haikubaliki.
 
Wananyimwa si kwa sababu ya "uharam" wao bali kwa sababu ya makosa ya wazazi wao. Kumbe si uharamu ndo unaowakosesha urithi bali ni makosa ya wazazi wao ndiyo yanawafanya wanyimwe urithi.
 
Mimi sina ndoa na nina mtoto, sasa mpumbavu gani mwenye haki ya kumuita mtoto wangu haramu? watu wanapapatikia mafundisho ya dini hata wasizozijuwa kujitungia maneno ya kifara kabisa.
Dini zimejaa utapeli mtupu kuja kufarakanisha watu weusi wasiojuwa lolote ili wachukiane kwa kigenzo cha huyu amafuata dini ya waarabu na huyu anafuata dini ya wazungu. ujinga mtupu.
 
Wananyimwa si kwa sababu ya "uharam" wao bali kwa sababu ya makosa ya wazazi wao. Kumbe si uharamu ndo unaowakosesha urithi bali ni makosa ya wazazi wao ndiyo yanawafanya wanyimwe urithi.
Unajuwa hapa naogopa kuwakwaza wale wanaomini dini za kurithisha mali watoto, hivi mtu unakaa chumba kimoja cha kupanga utaacha urithi gani dunia hii?
Na kwa nini ifikiriwe kwamba watoto kazi yao ni kurithi tu na sio wao kumiliki mali na wazazi wao ndio waje kurithi kama mtoto ataanza kufariki?
Hizi dini msizifuate kama misukule, changanyeni na akili zenu.
 
Mi naona si halali ingawa hatuwezi kupinga ukweli kwamba wakati mwingine mambo tunayofanya yanaweza kuwaathiri wale tunaowapenda.

Ila Hongera thread yako makini na ina mafunzo.
Tuna hitaji thread nyingi makini na zenye kugus
a maisha halisi ya watu.Sio kila siku wanawake sijui makalio kama watoto wa sekondari .
 
Hakuna mtoto wa haramu wala mtoto wa nje, wote watoto halali. haramu ni wale walioamua kuruhusu ushoga
 

Kwa hiyo unaajitangaza ili tujue kuwa ni jinsi gani ulivyo kubuhu kwenye uzinifu?
 
Kwa hiyo unaajitangaza ili tujue kuwa ni jinsi gani ulivyo kubuhu kwenye uzinifu?
Ni wapi nilipokutangazia kwamba mimi nimekubuhu kwa uzinifu? usinilazimishe mimi kuishi kwa imani unayoifuata wewe, ok, mimi ni muumini wa dini yangu ya kale ya mababu zangu, dini zetu za ukristo na uislamu usidhani kila mtu anaendeshawa na hizo imani zenu mlizoletewa wakati wa biashara ya utumwa.
Hao waliowaletea dini zao sidhani kama wanamjuwa mungu, maana haingii akilini kuleta dini sambamba na biashara ya utumwa. Heshima ni kitu cha bure.
 

Tatizo lako unakuwa na jaziba kwa kitu usicho kielewa! Urithi,ni haki ya mtoto pale inapotokea mmoja kati ya wazazi wake wawili au wote kufariki.

pamoja kuwa kurithi ni haki yake, haimzuwii yeye kutokutafuta mali yake. Na hata kama atakuwa anamiliki mali yake,ile haki ya kurithi bado itakuwepo. Kumbuka urithi si lazima warithiwa wawe wameacha nyumba,magari na vinginevyo. Hapana hata kama umeacha kijiko.

hebu nikupe mfano mdogo tu. Bwana Matola,inawezekana unamiliki mali na bahati mzuri,umebahatika kuwa na mtoto mmoja. Je iwapo utakuwa umetangulia mbele za haki ni sahihi mali zile ulizoziacha kumilikiwa na mtu yoyote from no where? Je ungependa zibaki kwenye miliki ya nani?
 

Nimetoa angalizo mapema kwamba hapa sitaki nimkwaze mtu kwa imani yake, lakini wewe unataka kuniondowa kunipeleka kwenye imani yako bila mimi kupenda.
Ni hivi kama dini yako inakuongoza uwe na mahakama ya kadhi kwa ajili ya mirathi hiyo ni juu yako na mungu wako, mimi imaani yangu inaniongoza kumuwezesha mtoto mapema, na kurithi mali zangu mimi naweza kulithisha charity yoyote ile na familia yangu isipate chochote..
Kwahiyo uelewe mimi sio muumini wa Mirathi.
 
Tuseme kwa faith ya wale waaminio mtoto wa kando, ni waharamu itabaki kua hivyo katika slogany but nijuavyo mie Baba still atakua responsible ku'provide frm A-Z juu ya huyo mtoto wa kando ecxept urithi ndiyo hatorithi, na hapo ndiyo source ya uharamu ilipoanzia.
Yaani mtoto wa kando kupata mirathi ya Baba ni haramu lakini kumridhi mama yake sio haramu.
Na Baba kumlea mtoto wa kando si haramu na niwajibu wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…