Ni hali ya kushangaza sana iwe kwa vijana au wapinzani kutukana tume

Ni hali ya kushangaza sana iwe kwa vijana au wapinzani kutukana tume

PeterwaPerer

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2024
Posts
292
Reaction score
336
Tume ya Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Jaji Chande akizungumza na wahariri na vyombo vya habari amenukuliwa akisema baada ya kutoa ripoti wamepokea matusi zaidi ya 300

Ni hali ya kushangaza sana iwe kwa vijana au wapinzani kutukana tume

Watu hawa ni wale wasiojijua hata jinsia zao, ni watu waliomezeshwa vitu bila kujua wanawanufaisha wachache ambao wanawatumia kupata malipo manono kutoka kwa watu wa nje

Yawezekana pia ni maroboti ya kikundi cha watu wenye hofu ya kukumbwa na jinai waliyoifanya tarehe 29th October

Lakini kama ni baadhi ya Watanzania wa kawaida, hakika hii nchi inahitaji kuponywa hata kwa mkono wa chuma!
 
Hayo malipo toka nje yanapitia wapi? BOT? Airport? Bandarini? Mpesa? Wire transfer, cash? Na watawala wapo wapi wakati yanapitishwa? Usiendelee kudhalilisha mamaduro na report yake kwamba mafunzo ya usaliti yalifanyika na mapolisi, majeshi, migambo, tissue, na kmkm wapo tu wamezubaa
 
Mengine yanapitia bandari bubu nadhani, siku moja Heche aliwahi kunukuliwa akisema anaijua vzr Mara hivyo angeamua kupita njia za panya asingekamatwa

Hata hela hizi nadhani zina njia nyingi za panya ili kuingia
 
Kama wao walivyo fanya eehhh
downloadfile-4.jpg
 
Tume ya Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Jaji Chande akizungumza na wahariri na vyombo vya habari amenukuliwa akisema baada ya kutoa ripoti wamepokea matusi zaidi ya 300

Ni hali ya kushangaza sana iwe kwa vijana au wapinzani kutukana tume

Watu hawa ni wale wasiojijua hata jinsia zao, ni watu waliomezeshwa vitu bila kujua wanawanufaisha wachache ambao wanawatumia kupata malipo manono kutoka kwa watu wa nje

Yawezekana pia ni maroboti ya kikundi cha watu wenye hofu ya kukumbwa na jinai waliyoifanya tarehe 29th October

Mbona ye katukana¿¿

Lakini kama ni baadhi ya Watanzania wa kawaida, hakika hii nchi inahitaji kuponywa hata kwa mkono wa chuma!
Kweli anahitaji kuponywa huyu
 
Haya yoote yanatokana na ile ripoti kuwa siri , ingewekwa wazi naona presha ingepungua sana.
1:Kusema zile picha za Gaza wee kuweza kuvumilia jambo km hilo. Kweli.
2:Kusema kuna watu walifadhili yale maandamano mmh ngum kumeza ujue.
3: Hizo training zikofanyikia bila kusema sehemu husika miye ngachoka.
4:Silaha walizobeba waandamanaji weee kuziona
.......Mengine malizia wewe ndiyo maana watu kuntukana Ndecha na hiyo tuuuumeee bwana in mpemba voice.
 
20260425_044405.jpg
Nadhani wewe utakua miongoni wa wajumbe wa tume ya "Chande na Machande" wenzake umekuja kujitetea .

Nikueleze tu wajinga waliisha aina ya propaganda mnazopiga zilitumika 1970 na kwa sasa haziwezi kufanya kazi.

Hivi kwa akili yenu mnaaamini vikundi vya kulipwa kupigana mnaweza kuvizima kwa siku 3 tu ??

Kwamba mafunzo ya kuandamana yalitolewa siku 28 msituni ?? huu ujinga nani mwenye akili timamu ataupokea?

Niwahakikishie tu kama watu wangepewa mafunzo ya kuandamana na wangekua na silaha kweli wala zile siku 3 za kuua watu wasio na silaha zisingefanikisha kupoza hali ya nchi ingechukua mwezi hadi miezi pengine mwaka hasa ukizingatia majiji yote na mikoa kadhaa ilikua na maandamano.

Hebu wekeni picha ya mwandamanaji hata mmoja mwenye bunduki au bomu kama mlivyodai .

Swali moja kuu ambalo hamjalijibu, hamuwezi kulijibu na hamtalijibu ni nani aliua watu zaidi ya 100000 ambao mmepika na kushusha hadi 518!

Pole mjumbe meli imeshang'oa nanga .
 
Hayo malipo toka nje yanapitia wapi? BOT? Airport? Bandarini? Mpesa? Wire transfer, cash? Na watawala wapo wapi wakati yanapitishwa? Usiendelee kudhalilisha mamaduro na report yake kwamba mafunzo ya usaliti yalifanyika na mapolisi, majeshi, migambo, tissue, na kmkm wapo tu wamezubaa
Chande na Juma wameharibu sifa za mtu kuitwa Jaji, majaji wanaonekana hawana tofauti na machawa
 
Mleta mada, kama angekuwa na umakini wa akili japo kwa kiwango kidogo, angetuambia kwanza na hao waliokuwa wanawaua watanganyika walilipwa na nani, walilipwa na na watu wa nchi gani? Angetueleza pia na walioanfika hiyo takataka inayoitwa report ya uchunguzi walilipwa na watu wa nchi gani kuandika huo uwongo wote, na ni kwa faida ya watu gani.
 
Chande na Juma wameharibu sifa za mtu kuitwa Jaji, majaji wanaonekana hawana tofauti na machawa

Majaji wenyewe kama ndio wa aina hii, ni afadhali tusiwe na mahakama, turudi kwenye mabaraza ya usuluhishi ya jadi. Hawa wamedhihirisha kuwa mtu akiwa mdhulumaji wa haki, akiwa tapeli, akiwa mhuni, kamwe elimu haiwezi kumwondolea tabia zake chafu alizo nazo, elimu aliyoipata ataitumia katika kuimarisha tabia zake ovu.
 
Chande alipataje hiyo nafasi ya kuwa Judge? Sijawahi kuona Judge mpumbavu kama Chande, hii mizee ndio chanzo cha umaskini na kudharaulika mtu mweusi,hana tofauti na kina mwijaku
 
Chande na Juma wameharibu sifa za mtu kuitwa Jaji, majaji wanaonekana hawana tofauti na machawa

Hii inacut accross taaluma zote ndani ya serikali, ni idara gani ndani ya nchi tunaweza kujivunia angalau inaonyesha professionalism tangu utawala wa Jekee? Umahiri mchache uliobaki uliondoka na Mkapa

Tusaidiane angalau moja tu tuipe maua yake!
 
Back
Top Bottom