Ni hatari sana kwenda au kuishi Kariakoo

Ni hatari sana kwenda au kuishi Kariakoo

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
14,311
Reaction score
36,056
Kwa ujumla mimi siendagi Kariakoo

Siyo sehemu salama, watu ni wengi sana, hakuna parking and kuna high level of noise pollution

Ukiacha hayo matatizo madogo madogo, magorofa mengi yaliyojengwa ni ya mchongo, huwa wanaweka load kubwa sana huko magorofani.

Kuna uwezekano mkubwa sana magorofa mengi yaka snap na kukawa na taharuki nyingine zaidi ya hii iliyotokea hapo juzi

Kimsingi, Kariakoo ni hazardous place, ukiwa unaenda mara kwa mara ni hatari sana

Nini kifanyike:

Serekali itafute alternative market place iwahamishie wafanyabiashara wote isipokua wa nguo na magodoro.

Hayo magorofa ya mchongo yahifadhi nguo na magodoro ambavyo siyo vitu vizito sana

Biashara nyingine kama hardware and spare parts ambazo ni nzito zipelekwe sehemu nyingine ili hayo magorofa ya mchongo yapumue na uhai wake uongezeke
 
Yaani sehemu hata parking ya pikipiki hamna let alone ya magari. kila sehemu watu wameweka meza au bidhaa. kwakweli hapako vizuri ni basi tu umaskini wetu tunakwenda kufuata bidhaa za bei rahisi.

Kuna watu kariako hawagusi kabisa.
 
Na Mbunge na wadiwani wapo
 
Kuna hapo opposite na chuo Uhasibu yale maghorofa yalishabomolewa au bado yapo ? Nilikuwa nahofu nikipita pale enzi zile. Kuna
Ukiingia Huko kwa akina kanjibahi PARISH nao ule mtaa unaghorofa zilichoka.Kiujumla DSm maghorofa mengi ni mabovu. Hameni mje huku porini muwe mnavuta hewa ya miti na mito.
 
Yaani sehemu hata parking ya pikipiki hamna let alone ya magari. kila sehemu watu wameweka meza au bidhaa. kwakweli hapako vizuri ni basi tu umaskini wetu tunakwenda kufuata bidhaa za bei rahisi.

Kuna watu kariako hawagusi kabisa.
Ukiingia mall kununua nguo hautatamani kwenda kkoo kununua nguo.

Shida ni umaskini tu kama unavyosema mkuu.
 
mimi nilikoma kwenda Karikaoo inafika miaka mitano, limekuwa ni eneo la ovyo sana wamachinga na bodaboda kila kona. Hakuna parking wala njia za watembea kwa miguu ni eneo ambalo wahuni tu na watu waliokosa ustaarabu wanaweza kuingia
 
Biashara ya Tz IPO kariakoo na ndo inaendesha nchi , nadhani kikubwa ni kuangalia namna ya kufanya maboresho zaidi .
 
Wakague hayo magorofa na wakikuta ya mchongo yabomolewe, waanzie na lile la Simba Sports Club 😂
 
Back
Top Bottom