Uchaguzi 2020 Ni hatua zipi za kisheria ambazo Tume (NEC) ina mamlaka dhidi ya mgombea anayetaka kusababisha uvunjifu wa amani?

Uchaguzi 2020 Ni hatua zipi za kisheria ambazo Tume (NEC) ina mamlaka dhidi ya mgombea anayetaka kusababisha uvunjifu wa amani?

Bado anaweza kuenguliwa kwa kukiuka kiapo alichoapa mbele ya mahakama kuu kwamba atazingatia maadili ya kampeni kama zilivyowekwa kwa mjibu wa sheria. NEC ndiyo ilimteuwa na ina mamlaka ya kutengua uteuzi wake wakati wo wote. Uamuzi wake hauwezi kupingwa mahakamani. Na huyo mgombea analijua hilo. Na anataka iwe hivyo ili akawaeleze waliomtuma kwani anajuwa hawezi kupata kura zaidi ya laki moja. Hawezi kuzunguka nchi nzima na hako kamtumba ka helikopta kenye pilot mwenye umri wa miaka 80. Nchi yetu ni kubwa kuliko ukizijumulisha nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kwa pamoja. Hawezi.
Kamwengue kama una uwezo huo. Unaacha mtu mwenye kauli mbovu za ukabila, unamkazania mtu anasisitiza NEC itende haki. Nosense.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Neno mabeberu limewakaa sana midomoni mwenu kama mlivyo karirishwa. Lakini mkiulizwa hao mabeberu ni akina nani hasa hamtoi majibu. Hamna tofauti na kasuku kuimba kitu usichokijua.
Mabeberu ni hao watu waliokuwa wanachukua maliasili zetu bure. Ni wanyonyaji wa mali zetu. Wanataka warudi tena kupitia mgombea huyu ambaye ameshawaahidi kwenye ilani yake: madini yetu atayaweka rehani ya mikopo watakayotupatia na riba yake, atawapa bure miradi ya sgr, bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere, mradi wa maji wa Ziwa viktoria na miradi yote aliyoanzisha Magufuli. Atavunja muungano wa JMT ili awape Zanzibar waimiliki kuweka submarine za majeshi yao. Kawahakikishia haki ya mapenzi na ndoa za jinsia moja. Kawahakikishia lugha yao ya kiingereza ndiyo itakuwa lugha ya taifa. Kawahakikìshia uhuru wa vyombo vyao vya habari nchini kwetu. Na kadhalika.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiingia Geita kwenye kampeni, Wenye wivu wajinyonge.
 
Kuna kanuni zilizowekwa kwa mjibu wa sheria ya uchaguzi wa namna ambavyo wagombea wanatakiwa kuzifuata wanapofanya kampeni kushawishi kura za wananchi. Kabla ya kuteuliwa na NEC wagombea hawa waliapa mbele ya mahakimu au majaji kuwa watazingatia kanuni na maadili hayo yaliyowekwa kwa mjibu wa sheria.

Kuna mgombea fulani ambaye ni wazi kabisa katika kampeni zake hazingatii kabisa hizo kanuni, taratibu na maadili aliyoapa kufuata. Lugha na maneno anayotumia dhidi ya mgombea mwenzake hayakubaliki hayakubaliki hata kidogo na ni kinyume na maadili yaliyowekwa na sheria hiyo. Ni maneno makali yenye kuuzi, kufedhehesha na kumudhalilisha (defarmatory) mgombea mwenzake.

Anatumia lugha ya kibabe yenye kuchochea uvunjifu wa amani. Amekuwa akirudia rudia kuwa ana watu wengi nyuma yake (wafuasi wake) na kwamba wasijaribu kumugusa maana moto watakaouwasha hakuna atakaye weza kuuzima. Bahati nzuri wale wa upande mwingine wamejitahidi sana kuwa wavumilivu na wastaarabu.

Sasa ni nani mwenye mamlaka ya kutiepusha tusifike pabaya? Jee Tume yetu ya uchaguzi inayo mamlaka ya kumchukulia hatua zipi za kisheria mtu kama huyu? Jee ina mamlaka ya kumpa onyo kali, karipio au kufuta uteuzi wake wa kuwa mgombea kabla hajawasha huo moto anaousema?
Lala, acha ujinga
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hiyo tume ya mgombea inapata wapi mamlaka ya kuengua wagombea wengine kwa jinsi tume ilivyojichanganya lolote itakalofanya halitakubaliks hapo isubiti uchaguzi tu. Kama ni kanuni zipo zile za kutotumia Lugha nyingine zaidi ya kiswahili hivi yule aliyekiuka wazi wazi na kusema wakichagua asiye wa chama chake hatapeleka maendeleo ndiyo kanuni za uchaguzi zinaruhusu hayo kuwatishia wananchi kuwa lazima wamchague mtu aliyempitisha yeye na kuacha aliyepitishwa na wananchi ndiyo kanuni zina sema wagombea wawachagulie wananchi muwakilishi wao
 
Tuombe tarehe 28 Oktoba 2020 ifike haraka ili wale wakuchechemea waendelee kuchechemea na wale wa kuzimia waendelee kuzimia! Na hata wale watandika konyagi waendelee kuitandika.
 
👊🏽👊🏽👊🏽👍🏽Ahsante sana Mkuu.

Sidhani kama NEC ina uwezo wa kumchukulia hatua Rais Magufuli kwa kuibua hisia za ukabila na ukanda kwenye kampeni, jambo ambalo ni kosa kubwa kwa sheria zetu.

Mtu anayeegemea kwenye ukabila na ukanda, ni hatari sana kwa amani ya nchi yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lazima uwe mjinga hasa kuamini kwamba siasa za ukabila na ukanda, siyo hatari kwa amani ya nchi yetu.

Mwalimu alifanya jitihada kubwa, na hakuwa na huruma na yeyote anayeendekeza siasa za kikabila, ukanda hata dini lakini leo inaonekana ni sifa kuegemea kwenye ukabila na ukanda. Na kuna wayu waendawazimu hawaoni hiyo kama ni hatari.

Unadhani kutatokea nini kwa mfano, Lisu naye akaenda mikoa ya kati, Kaskazini, Kusini, Nyanda za juu Kusini na Pwani, akawaambia kuwa Magufuli ameomba wasukuma wamchague kwa kuwa ni msukuma mwenzao, ninyi mtamchagua kwani ninyi ni wasilukuma wenzake? Nichagueni mimi kwa sababu mimi silitegemei kabila langu bali nategemea kura za ninyi Watanzania wote. Unadhani reaction ya wasio wasukuma itakuwaje?

Na je, baadaye hakutatokea kuchukiana au kupendana kwa misingi ya kikabila?

Kauli ya Rais Magufuli ya kusema, wasukuma nichagueni mimi msukuma mwenzenu na ni wa huku huku ilikuwa mbaya kabisa, na isiyostahili kutetewa na mtu yeyote mwenye upendo na Taifa letu.

Rais Magufuli atuambie, baada ya kuwaomba wasukuma wamchague kwa vile ni msukuma mwenzao, hahitaji kura za sisi wote tusio wasukuma?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sikushangai kwa Vihoja hivyo ulivyojenga tuamini kuwa kuna mgombea anatumia ukanda/ukabila kutafuta kura. Unayemtuhumu ni yuleyule amekuwa akitumia lugha zote za makabila ya nchi hii anazozimudu kuwasiliana na WaTz wakati wote alipokuwa madarakani. Iweje leo alaumiwe? Akitumia Kiswahili amekuwa akishutumiwa hajui Kiingereza! Upumbavu tu wa kuleta Vihoja
 
Kuna kanuni zilizowekwa kwa mjibu wa sheria ya uchaguzi wa namna ambavyo wagombea wanatakiwa kuzifuata wanapofanya kampeni kushawishi kura za wananchi. Kabla ya kuteuliwa na NEC wagombea hawa waliapa mbele ya mahakimu au majaji kuwa watazingatia kanuni na maadili hayo yaliyowekwa kwa mjibu wa sheria.

Kuna mgombea fulani ambaye ni wazi kabisa katika kampeni zake hazingatii kabisa hizo kanuni, taratibu na maadili aliyoapa kufuata. Lugha na maneno anayotumia dhidi ya mgombea mwenzake hayakubaliki hayakubaliki hata kidogo na ni kinyume na maadili yaliyowekwa na sheria hiyo. Ni maneno makali yenye kuuzi, kufedhehesha na kumudhalilisha (defarmatory) mgombea mwenzake.

Anatumia lugha ya kibabe yenye kuchochea uvunjifu wa amani. Amekuwa akirudia rudia kuwa ana watu wengi nyuma yake (wafuasi wake) na kwamba wasijaribu kumugusa maana moto watakaouwasha hakuna atakaye weza kuuzima. Bahati nzuri wale wa upande mwingine wamejitahidi sana kuwa wavumilivu na wastaarabu.

Sasa ni nani mwenye mamlaka ya kutiepusha tusifike pabaya? Jee Tume yetu ya uchaguzi inayo mamlaka ya kumchukulia hatua zipi za kisheria mtu kama huyu? Je, ina mamlaka ya kumpa onyo kali, karipio au kufuta uteuzi wake wa kuwa mgombea kabla hajawasha huo moto anaousema?
usimsahau na yule aliyetoa rushwa ya ajira elfu 13 na kujenga barabara 46km akiwa katikati ya kampeni.

hapa mi naona wote hao waenguliwe abaki Hashimu Rungwe peke yake tuogelee kwenye beche siye!😀😀😀😀😀

on a serious note, NEC haiwezi kum disqualify mgombea kwa kigezo ulichokisema huku ikifumbia macho kosa la kubwa kabisa la utoaji rushwa ambalo si tu ni kukiuka kanuni za uchaguzi bali ni jinai pia.
 
Sikushangai kwa Vihoja hivyo ulivyojenga tuamini kuwa kuna mgombea anatumia ukanda/ukabila kutafuta kura. Unayemtuhumu ni yuleyule amekuwa akitumia lugha zote za makabila ya nchi hii anazozimudu kuwasiliana na WaTz wakati wote alipokuwa madarakani. Iweje leo alaumiwe? Akitumia Kiswahili amekuwa akishutumiwa hajui Kiingereza! Upumbavu tu wa kuleta Vihoja
Kumbe u kilaza namna hiyo?
Kutumia kilugha kusalimia ni tofauti n kutumia kilugha kujinadi au kuomba kura kwenye eneo la kabila lako.
Kutisha watu kuwa wakichagua upinzani hutawapelekea maendeleo ni zaidi ya disqualification ya uongozi.
 
Unajifanya hujaelewa ni nani anayetaka kuwasha moto? Of course vyombo vya habari vyenye uzalendo haviwezi kuandika au kurusha maneno yake ya kutaka kuvuruga amani yetu. Ila NEC tunadhani inatakiwa kumuadabisha mtu huyu mapema iwezekanavyo kabla hajatuvurugia amani yetu. Kwanza anajua fika kwamba hatashinda uchaguzi; ije mvua au lije jua. Katumwa na mabeberu kuja kutuvuruga ili mabeberu warudi kupora natural resources zetu.
Natural resources wewe na nani?
 
Sidhani kama NEC ina uwezo wa kumchukulia hatua Rais Magufuli kwa kuibua hisia za ukabila na ukanda kwenye kampeni, jambo ambalo ni kosa kubwa kwa sheria zetu.

Mtu anayeegemea kwenye ukabila na ukanda, ni hatari sana kwa amani ya nchi yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wasiwasi wako tu, hakuna ukabila pale,
 
Kumbe u kilaza namna hiyo?
Kutumia kilugha kusalimia ni tofauti n kutumia kilugha kujinadi au kuomba kura kwenye eneo la kabila lako.
Kutisha watu kuwa wakichagua upinzani hutawapelekea maendeleo ni zaidi ya disqualification ya uongozi.
Mbona tundu anatisha watu kuwa wakimchagua magufuli watapata tabu kwani ana mpango wa kujiongezea kipindi kingine?
 
Kumbe u kilaza namna hiyo?
Kutumia kilugha kusalimia ni tofauti n kutumia kilugha kujinadi au kuomba kura kwenye eneo la kabila lako.
Kutisha watu kuwa wakichagua upinzani hutawapelekea maendeleo ni zaidi ya disqualification ya uongozi.
Hiyo siyo hoja ni Kihoja

Ukweli upo wazi kuwa viongozi wa upinzani, waliochaguliwa na wananchi, walipinga maendeleo na wamekuwa hawashirikiani na Serikali katika Majimbo na Kata walizoongoza. Walisusia vikao vya Bunge na kupinga bajeti.

Hivyo basi, ni sahihi wapiga kura kukumbushwa athali za kuchagua mgombea upinzani, kama wanahitaji maendeleo ya "vitu" ili yawawezeshe kujiendeleza.

Vipi na anayemkejeli mgombea mwenzake, yeye yuko sahihi?
 
Lengo lako wewe ni lipi ktk hili.
Bado anaweza kuenguliwa kwa kukiuka kiapo alichoapa mbele ya mahakama kuu kwamba atazingatia maadili ya kampeni kama zilivyowekwa kwa mjibu wa sheria. NEC ndiyo ilimteuwa na ina mamlaka ya kutengua uteuzi wake wakati wo wote. Uamuzi wake hauwezi kupingwa mahakamani.

Na huyo mgombea analijua hilo. Na anataka iwe hivyo ili akawaeleze waliomtuma kwani anajuwa hawezi kupata kura zaidi ya laki moja. Hawezi kuzunguka nchi nzima na hako kamtumba ka helikopta kenye pilot mwenye umri wa miaka 80. Nchi yetu ni kubwa kuliko ukizijumulisha nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kwa pamoja. Hawezi.
 
Kamwengue kama una uwezo huo. Unaacha mtu mwenye kauli mbovu za ukabila, unamkazania mtu anasisitiza NEC itende haki. Nosense.

Sent using Jamii Forums mobile app
NEC imuengue tu, hasa yule anayeomba kura kwa misingi ya kikabila hususan kufanya campaign akitumia lugha ya kabila lake badala ya lugha ya taifa.
 
Back
Top Bottom