Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Hili nililiona mapema kabisa hata kabla ya uchafuzi mkuu wa OCTOBER 29 2025
Katika mkanganyiko wa kupoteza madaraka ccm wakafanya waliyofanya na matokeo yake yakaonekana wazi dunia nzima
Kwa namna yoyote ile baada ya maandamano yale yaliyopelekea uharinifu wa mali mauaji ya kutisha, ukatili mkubwa kwa waliokamatwa isingewezekana kwa vyovyote vile kuweza kufanya sherehe za uhuru wa Tanganyika
Hali bado ni tete sana hata kaka kusingekuwa na maandalizi ya maandamano ya Dec 9 siku ya uhuru
Kama baada ya uchafuzi uapisho ulifanyika chini ya ulinzi mkali kwenye kambi ya jeshi.. Isingewezekana kwa namna yoyote ile kukusanya wananchi wakahudhurie sherehe za uhuru tena ndani ya kipindi kifupi cha kisichofika hata miezi miwili
Hekima imetumika kwa sababu za wazi kabisa.. Lakini busara ingekuwa kuziweka wazi kuliko kudanganya uma na kutoa visingizio vya kitoto
Sababu ya kusema eti sherehe zitafutwa na bajeti yake kupelekwa kukarabati miundombinu iliyoharibika kwenye maandamano inakera Sana
Je imeshajulikana tayari bajeti ya kukarabati ni bei gani na bajeti ya sherehe za uhuru ni bei gani?
Kwani taasisi inayohusika na miundombinu haina bajeti yake ya fharura kwenye majanga ya asili na ya kibinadamu?
Je utaratibu wa kikatiba umefuatwa kwenye kuzifuta sherehe ama matamko ya wanasiasa yanatosha?
Ilipaswa kutamkwa wazi kwamba kwa yaliyotokea October 29 kwa namna yoyote ile haingekuwa busara kuwa na sherehe za uhuru
Kiutu
Kijamii
Kiungwana
Kiusalama
Kiimani nk
Watu kwa maelfu hawajamaliza hata arobaini za wapendwa wao. Mtu atapata wapi uthubutu wa kufanya sherehe?
Shida kubwa inayoitesa Tanganyika ni mamlaka kushindwa kuongea ukweli penye ukweli na uhalisia penye uhalisia
Siku zote ni kutumia kanuni ya mbuni ya kuzika kichwa ardhini ili asionekane na ile ya kufunika kombe mwanakharamu apite!
Good morning Tanganyika⚡☄📌🔨