Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,518
- 10,839
Jana ndiyo nimeamini ni heri utupe nyavu halafu ukataliwe kuliko kuishi na majuto baada ya kutotupa nyavu.
Jana nilikuwa nasafiri kutoka mkoa X kwenda Z kwenye basi nilikaa na binti mmoja alikuwa mchangamfu kweli, tulipiga stori za hapa na pale mpaka alipofika anaposhukia, alikuwa anashukia njiani, basi akaniaga na kuniuliza "kwahiyo utarudi lini mkoa X?" nikajibu "nitakuwepo mkoa Z kwa muda mrefu" akajibu "aah sawa, safari njema" huku akichukua begi lake la mgongoni na kushuka.
Sasa stori ya huu uzi inaanzia wakati nakaribia mkoa Z kwakuwa ilikuwa saa 10 nikapata wazo nikishuka stendi nisiende moja kwa moja ninapoishi badala yake niende katikati ya mji nikale chakula kwanza ndiyo niende nyumbani.
Basi nilipofika tu mkoa Z moja kwa moja nikaenda kwenye mgahawa mmoja maarufu, wana chakula kizuri. Nikakuta foleni moja kubwa sana, nikaona meza moja ipo tupu nikachukua soda na kwenda kukaa, kwa ile foleni nikabadili mawazo na kutoa order ya chakula ila wanifungie ili nibebe.
Ukapita muda kidogo, akaingia mtoto mmoja mkali sana, nikisema pisi kali ndiyo naeleweka zaidi: hapa namaanisha pisi kali kwelikweli kwasababu macho yangu hayajawahi kudanganya. Pisi flani black (mambo yangu kabisa) mrefu, sura ipo (wenyewe wanaita face card) umbo no. 8. Akakaa kwenye meza niliyokuwepo na tukawa wawili tu pale, akanisalimia, nikaitikia: muda wote huo ni kama nimepigwa shoti kimoyomoyo nikijisemea "she's way out of my league, damn!" nikapiga one sip ya Sprite yangu wakati nasubiria order yangu ya chakula lakini uzuri wake ukiendelea kuupa ubongo wangu kazi ngumu ya kuchakata taarifa ipasavyo.
Muda huo baada ya kuketi akiwa kwenye simu yake huku akisikiliza muziki kwenye airpords zake, mara kidogo akauliza "kaka samahani, wanaohudumia vinywaji ndiyo hawahawa wa chakula" nikajibu "hapana ni wale" huku nikimuonyesha, nikaongezea "au unaweza kwenda kuchukua kinywaji unachotaka kwenye fridge" basi, akanyanyuka na kwenda kuchukua Sprite 500ml nikajisemea kimoyomoyo "yes, now we're even, now how to break the ice?"
Muda huo ni saa 11 kasoro dk 10, nikakumbuka chama langu Manchester United linaingia mzigoni hivyo nikacheki line-up na mechi ilipoanza nikaanza ku-stream. Wakati mechi inaendelea akampigia mtu simu, nikawa makini: kwa yale maongezi nikahisi kama anaongea na mbunge mwenye jimbo lake, hapo ndiyo nikaona rejection hapa ni kugusa tu tena mbele ya kadamnasi.
Kiukweli ile mechi niliangalia kwa dk 23 tu maana nilikuwa sielewi kabisa kinachoendelea uwanjani. Kila nikipiga jicho mtoto katulia tu anasikiliza muziki, nikabaki na maswali tu "kwanini haagizi chakula au kuna mtu anamsubiria?" basi, order yangu ikawa tayari nikalipia nikaweka kwenye mfuko, nikalipia soda. Then, nikatulia kidogo maana kuna mtu nikawa nampigia aje anichukue pale nilipo ila hapatikani, muda wote huo akili inawaza tu "natupaje nyavu hapa?" Nilishahesabia kama a missed opportunity maana ule muda wakati ananiuliza ndiyo ilikuwa muda sahihi wa kuanzisha a long conversation.
Akilini nikakubali tu leo nimekuwa Darwin Nuñez maana 1v1 nimepaisha kabisa. Nikachukua mfuko wangu wa chakula na begi langu nikaburuza taratibu na kuondoka. Wakati naenda nyumbani sasa ndiyo akili ikaanza kukaa sawa: wanaongalia mpira huwa kuna msemo wetu maarufu pale mchezaji anaposhindwa kufunga goli rahisi "amekosaje pale?" hicho ndiyo nikawa najiuliza maana ni kama nilikuwa under pressure na nikapoteza composure kabisa.
Nimeshakuwa kwenye mahusiano na pisi kali ila hii ya jana nimenyoosha mikono maana hii ni GENERATIONAL FUMBLING. Baada ya miezi kadhaa kuwa single nimepoteza kabisa umakini nikiwa kwenye lango 1v1 na kipa tu.
Huu uzi nimeandika maana jana wakati naenda nyumbani nimejutia kwa ile nafasi niliyoipoteza maana sijui kama naweza kukutana tena na yule binti, leo nimeamka lakini bado tu nawaza nini kilitokea jana, nimeshindwa kabisa kupotezea.
Lengo la uzi huu ni kuwashauri wazee wenzangu wa kutupa nyavu, ni heri uombe namba usipewe au ukataliwe kabisa ila usipojaribu hata kidogo kutupa nyavu majuto yake hayaelezeki. Najua kuna watu watakuwa wameshawahi ku-experience hii kitu "FUMBLING" dah!
Shoot your shot, or prepare to live with regrets.