Inaendelea... Mida ikasonga foleni ikawa inasogea ila naona najiuliza mbona haniiti? Au nimgeukie? Je nikimgeukia nimwambie nini? Au maneno gani? Mwanaume nakosa majibu. Leo naionea aibu pisi kali iliyopo nyuma yangu. Nikaamua kuwa mpole ngoja nimalize kwanza kujiandikisha then niangalie namuingiaje huyu mdada.
nikiwa kwenye foleni nikaanza kupanga maneno ya kumuambia, ngoja nitamuuliza kama atakubali tukae mahali tuzungumze alafu mda unaelekea mchani ni vizuri tukapa lunch pamoja" Yote hayo nilikuwa nawaza.
ikafika zamu yangu kuingia ofsini kujiandikisha, yule mdada akawa kasimama mlango pale foleni inapoishia kusubiri atoke aliye ingia then nawe ndio uingie.
taratibu za kujiandikisha zikaanza naulizwa majina yangu matatu, mwaka wa kuzaliwa, kabila, majina ya wazazi, nk..
yule mdada akawa makini sana jinsi ninavyojibu yale maswali akiwa kasimama pale mlangoni, akawa ananiangalia sana hadi ilipofika mda wa kupiga picha passport niliyona aibu yaani itaendelea...