Ni Hospitali gani ya Umma (ya Serikali) hasa hasa Mkoani Dar es Salaam yenye Huduma Rafiki ya Kung'oa Meno?

Ni Hospitali gani ya Umma (ya Serikali) hasa hasa Mkoani Dar es Salaam yenye Huduma Rafiki ya Kung'oa Meno?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
63,685
Reaction score
128,178
Kuna moja hivi ipo jirani kabisa na eneo ambalo Mvua ya Dar es Salaam ikianza tu Kunyesha basi Utepe wa Usalama wa Barabara Kufungwa huwa unawekwa karibu na ilipo. Kuna Mtu alinishauri niende hapo Kung'oa ila nimefanya Survey yangu naona kila wanaoingia hapo wakitoka ama wanakuwa Wanalia sana au Wamekunja Nyuso zao kwa Hasira na wengine wakitoka Nduki (wakikimbia) kabisa.

Mkoa wa Dar es Salaam una Hospitali nyingi za Umma (Serikali) hebu nitajie Moja tu ambayo nikienda Kung'oa Jino nitatoka na Furaha tele tu.
 
Kama utakosa ya serikali basi nenda Morocco, inaitwa Dental Empire (ni dental Clinic).
 
Yaani nihonge Kung'olewa Jino / Meno? Sasa si bora nijenge tu Urafiki wa muda na Bondia Mwakinyo nimchokoze anipige Ngumi na Jino ling'oke?
UJENGE URAFIKI KISHA UMCHOKOZE? Hahahaaaa kweli we popoma. Hebu pita 94KJ WANAUME wakung'oe hiyo mi Ronaldinho.
 
Regency hospital wana huduma nzuri ila uwe na bima.
 
UJENGE URAFIKI KISHA UMCHOKOZE? Hahahaaaa kweli we popoma. Hebu pita 94KJ WANAUME wakung'oe hiyo mi Ronaldinho
Naishi jirani tu na Hospitali yao Kuu ila hata niambiwe wataning'oa bure siendi ng'o. Watu wanang'oa Jino kwa Hasira utadhani wanategua Bomu!
 
Regency hospital wana huduma nzuri ila uwe na bima
Kwa Umasikini (Ukapuku) wangu Tukuka kabisa GENTAMYCINE unadhani Mkuu nitakuwa na hiyo BIMA kama hata Kula yangu tu ya leo hii siijui?
 
Kuna wakati mnazi mmoja hospital ilikua bora sana kwenye kitengo cha mano na macho.
Hiki Kitengo cha Mano na Macho hapo Mnazi Mmoja Hospital ni Kipya au? Mano na Macho Department.
 
Chukua kijiti choma kwenye moto kikiwa chekundu king'ate na hilo jino linalo uma utanishukuru:

Powered by Dkt. Don Nalimson The next presidental..
 
Temeke hospital alikuwepo mama mmoja sina hakika kama bado yupo yule ni fundi sana yani haumizi kabisa. Ila siku nyingi nimepita sijaenda sijui kama bado yupo. Pia Mbagala maeneo ya kipatti kuna dr. Binafsi nae anatoa meno vizuri sana.
 
Nenda Muhimbili jengo la OPD karibu na jengo la wazazi wanang'oa meno vizuri sana.
 
Nenda Muhimbili mi nimetoa meno pale hakuna rushwa. Kuna fast track na kawaida. Fast track bei iko juu. Wanaotoa pesa wanataka fasta fasta hiyo ni juu yako.
 
Ila ujue meno yanatofautiana na magonjwa ya meno yanatofautiana pia, hivyo hata utoaji wa meno pia ni tofauti.

Usifikiri kama wewe ulitolewa jino bila tatizo basi na mwenzio atang,olewa pia kirahisi kama wewe

Kuna jino kitaalamu wanaita impaction, yanakuaga ni magego. Hili halitolewi kirahisi kama meno mengine ya kawaida. Kuna meno unakuta fizi zina shida haya yanatoka kirahisi sana.
 
Back
Top Bottom